.jpg)
Miti Katika Qur’an na Mazingira
(1)
na Ben Rijal
Miti ni maisha na maisha yetu yanategemea miti, itapotoweka
miti na mimea maisha ndio yatapomalizika, tunapata chakula chetu cha kila siku
kutokana na miti, sayari yetu hii hupozwa na miti, bahari, mito, maziwa n.k. nakuijaalia
kuweza kukalika.
Makala 3 mfululizo nitaizungumzia miti, makala ya
kwanza nitazungumzia baadhi ya miti iliotajwa katika Qur’an, makala ya pili
itazungumzia miti ya madawa katika Quran na makala ya mwisho itaangalia miti na
Mazingira.
Katika Qur’an imetajwa aina ya miti 54 kati ya hayo 3
haipo duniani, iliyobaki yote inaonekana duniani. Huko Dubai kumetengenezwa
bustani itwayo ‘Emirates Holy Qur’an
Park’ ambayo miti yote iliotajwa katika Quran itaoteshwa, hadi naandika
makala hii, miti 31 tayari imeshaoteshwa na 20 mengine itaoteshwa badaye na 3
nishakwisha kuelezea kabla kuwa haipo duniani. Bustani hii inategemewa
kufunguliwa rasmi mwezi wa 9 mwaka huu katika eneo la Al Khawaneej na kugharimu
Dh26 milioni.
Miti imetajwa kwa kujirudia katika Quran, kwa mfano
mti wa Mana umetajwa mara 3 katika Surah (2:57; 7:160; 20:80-81), Mtende
umetajwa mara 20 katika Surah 2:266; 6:99; 6:141; 13:4; 16:11; 16:67; 17:91;
18:32; 19:23; 19:25; 20:71; 23:19; 26:148; 36:34; 50:10; 54:20; 55:11; 55:68;
69:7; 80:29, Mizaituni imetajwa mara 6 katika Surah 6-99; 6-141; 16-11; 23-20;
24-35, Mzabibu umetajwa mara 11 katika Surah ((2-266; 6-99; 13-4; 16-11; 16-67;
17-91; 18-32; 23-19; 36-34; 78-31, 32; 80-28), Komamanga limetajwa mara 3
katika Surah 6-99; 6-141; 55-68, Tini imetajwa mara 1 Surah 95 :1, Mkunazi
umetajwa mara tatu 34:15-16; 53 : 14-18, 56 :28, Mkunazi kama Msuwaki
umetajwa mara moja 34 :16, Hena mara moja katika Surah 76 :5,
Mtangawizi umetajwa mara moja Surah 76 :17, Adesi imetajwa mara moja
katika Surah 2 :61, Kitunguu mara moja katika Surah 2:61, Kitunguu Thoumu
kimetajwa mara moja Surah 2 :61, Tango ujmetajwa mara moja Surah
2 :61, Mung’unye umetajwa ma ra moja katika Surah 37 :146, Khardali
umetajwa mara 2 katika Surah 21: 47; 31:16. Unapoisoma Qur’an kwa makini na
kuichambua katika fani mbalimbali utakuja kufahamu mambo ambayo ynaungana na
masuala mbalimbali iwe kilimo, mazingira, tabia n.k.
Zifwatazo ni aya ambazo zimeshehereshwa juu miti
katika Qur’an unapozisoma unaona utukufu wa Quran na maelezo yake.
Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika
Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu
tu; mkawa katika wale walio dhulumu. (Surah Al-Baqara, 35)
Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa
juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali,
na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake
inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo.
Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo. .
(Surah Al-An‘am, 141)
Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii,
na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio
dhulumu. (Surah Al-Aa‘raf, 19)
Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia
tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila
msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele. (Surah Al-Aa‘raf, 20)
Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti,
tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao
Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani
ni adui yenu wa dhaahiri? (Surah Al-Aa‘raf, 22)
Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, na
zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye
shina moja na isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Na
tunaifanya baadhi yao bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo
ishara kwa watu wanao tia mambo akilini. (Surah Ar-Raa‘d, 4)
Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano
wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako
mbinguni. (Surah Ibrahim, 24)
Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee
majumba yako katika milima,na katika miti, na katika wanayo jenga watu. (Surah
An-Nahl, 68)
Na tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha
wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndoto tulio kuonyesha ila ni kuwajaribu
watu, na mti ulio laaniwa katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakini
haiwazidishii ila uasi mkubwa. (Surah Al-Israa’, 60)
Lakini Shet'ani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe
Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi milele na ufalme usio koma? (Surah Taha, 120)
Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu viliomo
mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na
miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na
anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu
hutenda apendayo. (Surah Al-Hajj, 18)
Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na
mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula. (Surah Al-Muminun, 19)
Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta
na kuwa kitoweo kwa walao. (Surah
Al-Muminun, 20)
Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa
Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika
tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo
toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi.
Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya
Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu
huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. (Surah
An-Nur, 35)
Au NANI yule aliye ziumba mbingu
na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha
bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo
mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka. . (Surah An-Naml, 60)
Na
lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na
ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingeli
kwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (Surah Luqman, 27)
Lakini
wakaacha. Tukawapelekea mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani
zao hizo kwa bustani nyengine zenye matunda makali machungu, na mivinje, na
kidogo katika miti ya kunazi.
(Surah Sabaa, 16)
Sema:
Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.
(Surah
Ya Sin, 79)
Aliye
kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. (Surah
Ya Sin, 80)
Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa
Zaqqum? (Surah As-Saffat, 62)
Na
tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye. (Surah As-Saffat, 146)
Hakika Mti wa Zaqqum, (Surah
Ad-Dukhan, 43)
Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi Waumini
walipo fungamana nawe chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi
akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu. (Surah
Al-Fath, 18)
Baadhi
ya faida zitokanazo na miti: Miti hufanya kazi ya kunyonya gesi ukaa na
kutupatia gesi ya Okisijini ambayo tunaitegemea kwa uvuta pumzi, Mizizi ya miti
husaidia kuidhibiti udongo na kuepusha mmong’onyoko wa ardhi, Miti husaidia
kuboresha maji pale majiya
mvua yanavyopenya kwenye ardhi, Idadi inayotimia ¾ ya wakazi wa dunia
wanategemea kuni kwa maisha ya o ya kila siku ikiwa kuni zinatokana na miti,
Vitu visiopungua alfu hutengenezwa kutokana na zao la miti kutka fanicha,
makabati, viti, karatasi, mabao ya kuchezea mchezo wa hook na kriketi, ujenzi
wa nyumba n.k. Miti huitremesha hali ya joto, Miti hutoa chakula, kivuli na
makazi kwa wanadamu na wanyama, Miti huwakisaidizi ya kuzuwia sauti kali zenye
dhara aidha husaidia kuzuwia kasi za upepo, Miti huleta mandhari nzuri katika
maeneo mbalimbali.

Miti itoapo mandhari nzuri

Miti katika maeneo yake asili
No comments:
Post a Comment