Hamzah Z. Zubeir
Ibn Khaldun
Makumbusho
ya Ibn Khaldun huko Tunis
Ibn
Khaldūn (jina kamili kwa Kiarabu ni أبو زيد عبد الرحمن بن محمد بن خلدون الحضرمي Abū Zayd ‘Abdu r-Raḥman bin Muḥammad bin Khaldūn Al-Hadrami; mara nyingi kama Abdul Rahman
Ibn Khaldun) alikuwa mtaalamu Mislamu kutoka Afrika ya Kaskazini
alyieishi wakati wa karne ya 14. Alizaliwa mjini Tunis
mnamo 1332 akaishi baadaye Fez
na Granada na miaka ya mwisho alikaa Kairo
alipokufa 1406.
Kimaitaifa
anajulikana hasa kam mtaalamu bora wa historia. Lakini anatazamiwa pia kama
mtangulizi muhimu katika fani kama falaki, uchumi, fiq-hi, hisabati, elimu ya
jamii.
Yaliyomo
Taarifa Juu ya Maisha Yake
Aliandika
mwenyewe kitabu cha "at-ta'rif bi-Ibn Chaldun wa-rihlatuhu gharban
wa-scharqan / التعريف بابن خلدون ورحلته غربا وشرقا / taarifa ya Ibn Khaldun juu ya
safari zake za magharibi na mashariki". Hasemi mengi juu ya maisha yake ya
binafsi lakini anajieleza aliposoma, walimu wake na vitabu alivyosoma. Alikuwa
mtoto wa familia ya makabaila walioitwa "banū chaldūn"
walioishi miaka mingi huko Andalusia (Hispania ya
Kiarabu). Kiasili walitoka katika Yemeni. Wakati wa rekonkista
yaani kipindi ambako Wahispania wenyewe walianza kuwasukuma Waarabu kutoa
maeneo mengi ya nchi yao akina banu khaldun walihamia Afrika ya Kaskazini. Hapa
mababu kadhaa wa Ibn Khaldun walipata vyeo muhimu chini ya watawala Waislamu.
Babu na baba yake waliacha siasa wakajiunga na tarikat
ya Wasufi.
Masomo na Maisha
Kijana
Ibn Khaldun alisomeshwa na walimu bora wa Afrika ya Kaskazini akasoma qurani, lugha ya Kiarabu, ahadith,
fiq-hi, hisabati, mantiki na falsafa. Hapa alisoma hasa kazi za Ibn Rushd
(Averroes), Ibn Sina Avicenna, Razi na at-Tusi.
Alipokuwa na miaka 17 wazazi walikufa kutokana na ugonjwa wa tauni.
Alifuata
mapokeo ya familia akitafuta ajira serikalini kwa watawala malimbali wa Afrika
ya Kaskazini. Nia hii ilimpeleka katika maisha ya hatari yingi kwa sababu
wakati wake watawala walibadilika haraka wakiangushana na kuwa na vita kati
yao. Kwa hiyo Ibn Khaldun alipata vvyeo vikuu vilivyofuatwa na vipindi katika
jela na miaka alipopaswa kukimbia nchi yake.
Tunis, Granada na Afrika ya
Kaskazini
Ajira
ya kwanza ilikuwa kwenye ikulu ya mtawala wa Tunis
alipokuwa na miaka 20. Alipewa cheo cha kātib
al-ʿalāma
كاتب العلامة yaani karani na mwandishi aliyetoa
amri na matangazo rasmi ya sultani kwa maandishi mazuri.
1357 alitupwa jela kwa miezi 22 hadi sultani alikufa na mfuasi wake
alimrudishia cheo chake. Alipanda ngazi hadi kuwa katibu mkuu wa mtawala. Sultani
huyu alipopinduliwa aliondoka Tunis akaenda Granada ya Andalusia alipopokelewa
vema na amiri Muhammad
V aliyemfanya balozi wake kwa mfalme Mkristo wa Kastilia
Pedro I
akafaulu kupatana na mfalme a kupata mkataba wa mani kati ya Kastilia na
Granada. Baada ya kurudi Granada alionewa mafanikio yake na waziri wa amiri
akapaswa kuondoka tena akarudu Afrika ya Kaskazini.
Hapa
alitumikia watawala mbalimbali wa madola madogo ya Kiislamu katika eneo la Algeria ya leo. Baada ya kuchoka siasa akaenda
kuishi katika eneo la Waberber waliojitegemea
akaanza kuandika kitabu cha historia ya dunia kati ya 1374–1377. Lakini hapa
porini alikosa vitabu vya marejeo alivyohitaji kwa kazi yake akahamia tena
Tunis.
Sultani
mpya wa Tunis alimwajiri lakini Ibn Khaldun alikuwa na wasiwasi juu ya siasa
zake akaomba rukhsa ya kwenda hajj ya Maka kama mbinu wa
kuondoka Tunis akapanda jahazi ya kwenda Aleksandria katika Misri.
Misri
Misri
ilikuwa dola tulivu iliyokuwa na kipindi cha tawala imara na maendeleo ya
kiuchumi chini ya nasaba ya Mamaluki.
Tena Aleksandria ilikuwa kitovu cha elimu na hapa aliendelea na masomo na
utafiti wake. Lakini hata hapo alishindwa kukaa mbali na siasa kwa sababu mwaka
1384 sultani Barkuk alimteua kama profesa wa fiq-hi na qadi mkuu
kwa dhehebu la maliki.
Majaribio yake ya kuleta matengenezo katika fiq-hi jinsi Wamisri walivyozoe
yaligonga ukuta aliona upinzani na kujiuzulu bada ya mwaka mmoja pekee.
Hapo
aliamua kutekeleza nia ya awali akaenda kuhiji Maka. Baada ya kurudi kutoka
Maka akaendelea kufundisha kwenye vyuo vya Aleksandria akarudishwa tena kama
qadi kwa Wamaliki; alirudia kujiuzlu akarudishwa tena mara kadhaa kutokana na
sifa zake za utaalamu katika cheo ambacho hakupenda.
Mwaka
1401 aliamriwa kushiriki katika vita ya sultani mpya al-Nasir
Faraj dhidi ya Wamongolia
chini ya Tamerlan huko Syria
kama mshauri wa mtawala. Mjini Dameski Ibn Khaldun alijikuta
akifungwa ndani ya mji ulioshambuliwa na jeshi la Tamerlan. Ibn Khaldun
aliteuliwa na watu wa Dameski kwenda kama mbalozi wao mbele ya mtawala wa Wamongolia
na kuomba radhi kwa mji. Hapa alikutana mara kadhaa na Tamerlan na kujadiliana
naye juu ya mengi akaokoa mji mbele ya hasira yake.
1401
aliweza kurudi Misri alipoandika taarifa ndefu juu ya Wamongolia akaendelea
kukamilisha vitabu vyake juu ya maisha yake mwenyewe na juu ya historia ya
dunia.
Mwaka
1406 aliaga dunia mjini Alkesandria.
No comments:
Post a Comment