Tuesday, 7 April 2015

AZAM TV KARUME DAY: ABEID AMANI KARUME - "THE MASTERMIND" MAHOJIANO NA IRENE KILENGA




Picha hii ilipigwa Dar es Salaam mwaka 1948
Kushoto waliokaa Hassan Machakaomo, Selemani Mwinyimadi Chambuso, Mohamed ''Mabosti'' Sultan
Waliokaa kwenye viti kushoto wa kwanza jina halikupatikana, Rajab Swedi, Khamis Shari, Abeid Amani Karume, Kondo Salum Kipwata, Mtaruke Mangara, aliofuatia jina halikupatikana
Waliosimama Abdallah Mzee, Chonjo Mwinchande Digendo, Juma Ismail, Shaaban Bajuni, anaefuatia jina halikupatikana, Khamis Mjinga, Selemani Mohamed, Mtoro Rehani, Mangara Tabu Mangara, Ali Majaliwa
Hawa walikuwa viongozi wa Young Africans Football Club














Hapo ni leo asubuhi (7 Aprili, 2015) nikifanya kipindi maalum cha Rais Abeid Amani Karume (1905 - 1972) "The Mastermind," na Irene Kilenga wa AZAM TV. 

Kipindi kilikuwa cha takriban saa moja na nilieleza maisha ya Karume kuanzia mwaka 1955 alipohudhurua mkutano wa kwanza wa TANU uliofanyika Ukumbi wa Hindu Mandal Dar es Salaam ambako alikutana na Mwalimu Nyerere na Karume akamualika Nyerere Zanzibar. 

Nilieleza pia hiyo haikuwa ndiyo mwanzo wa kukutana. 

Walikutana kabla Zanzibar... 

Mtangazaji wa AZAM TV Irene Kilenga alivutiwa sana na jina nililompa Mzee Karume - "The Mastermind," na alitaka kujua zaidi ni kipi kilinifanya mimi kumpa jina hilo. 

Nilimpa kisa chake toka mwanzo 1955 hadi kumalizikia kuuliwa kwake 1972. 

In Sha Allah itakapopatikana DVD yake itawekwa...


Humud

Sala ya Jeneza


No comments: