Monday 18 May 2015

KUTOKA SAFU ZA FACEBOOK MJADALA WA TATIZO LA KUANDIKA HISTORIA AFRIKA



  • Mohamed Said Sheikh Ally ili uweze kuona matatizo ya historia yetu nakuwekea hapa niliyoandika kueleza historia ya TANU na jinsi mtu muhimu sana katika kuasisi TANU na uhuru wa Tanganyika alivyopotezwa katika historia hiyo. Huyu ni Abdulwahid Sykes. Hebu soma historia yake kwa uchache kama niliyoeleza katika mjadala: "Yericko, 
    Huijui historia ya TANU. 

    TAA haikuasisiwa 1927 bali 1929 na wakati ule nafasi za uongozi
    hazigombewi. 

    Msome Iliffe "Modern Tanzanians" Kleist Sykes the Townsman 
    (Daisy Sykes) (1973) historia nzima ya AA imeandikwa mle. 

    Nimekuwekea "note" ya JV kwa Edmund akieleza mkakati wa 
    Nansio kati ya Hamza Mwapachu na Abdul Sykes vipi wabadili 
    uongozi 1953. 

    Kuhusu uchaguzi wa 1950 uliowatia madarakani Abdul na Kyaruzi 
    msome Listowel (1965) "The Making of Tanganyika," utajifunza 
    mengi na utajua kuwa juhudi kubwa ya kuwaingiza vijana hawa 
    madarakani ilitoka kwa Schneider Abdillah Plantan na huyu 
    alikuwa mmoja wa baba zake Abdul na aliyekuwa ametolewa 
    madarakani alikuwa Mwl. Thomas Plantan kaka yake Schneider 
    kwa hiyo ni baba yake mkubwa Abdul.

    Hebu soma hiki kipande na mtafute Dr. Kyaruzi katika uongozi wa 
    TAA mwaka 1953 kabla TANU haijaasisiwa:

    Hayo hapo chini ni kutoka kitabu changu: "The Life and Times of 
    Abdulwahid Sykes..." (1998):

    In June, TAA headquarters announced its executive committee with 
    J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. 
    Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and 
    Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
    and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. 

    Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, 
    Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo 
    and Patrick Aoko.[1] 

    Yuko Kyaruzi hapo?

    Sasa ikiwa viongozi ndiyo hao 1953 mwaka mmoja kabla ya TANU 
    kuasisiwa Kyaruzi katoa mchango kutoka chama kipi na katika 
    mwaka upi?

    Mwisho tunarudi palepale tulipoanzia na mimi kupata sababu ya 
    kuandika kitabu ambacho kwa miaka sasa kila uchao tunakizungumza
    hapa jamvini.

    Ikiwa historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo hii na historia ya TANU 
    chama cha uhuru ndiyo hii...

    Imekuwaje historia ya TANU ikaja kuandikwa na ikawaacha nje wengi 
    wa wazalendo hawa?

    Inawezekana Yericko Nyerere akaja na jibu.

    Ningependa kumweleza Yericko kuwa Abdul alikuwa Kaimu 
    Rais TAA baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwira
    (ingawa Yericko anasema uhamisho ulikuwa Sengerema) na alikaimu 
    nafasi hiyo toka 1951 - 1953.

    Baada ya uchaguzi wa 1953 uliomuingiza Nyerere madarakani kama
    rais wa TAA Abdul akawa makamu wa rais.

    Unapoandika historia ya TANU na ukaanza na Nyerere na kumtoa nje 
    Abdul Sykes hapo mtafiti anakuwa kajipalia makaa.

    Historia hiyo haiwezi kusimama kwani mtafiti anakuwa si kama kajipunja yeye mwenyewe bali pia kaipunja historia ya uhuru wa Tanganyika.

    Jambo la kushangaza ni kuwa Dr. Kyaruzi alipatapo kueleza kuhusu
    historia yake ya siasa na akasema kuwa ilikuwa yeye ndiye aliyemwachia Nyerere chama.

    Katika makala nzima hakupata kumtaja Abdul Sykes wala uchaguzi wa
    1950 wala hakumtaja Schneider Plantan.

    Ilikuwa yeye Kyaruzi na Nyerere peke yao katika historia ya TANU.
    Hizi ndizo historia zetu. Sasa haiwezi kuwa ajabu kwetu sisi kuwa kuna watu wengi hawaijui historia ya Mapinduzi na wala hawajui Hanga alikuwa na mchango gani katika mapinduzi yale. Medali za Mapinduzi zimetoka katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi na jina la Hanga halikuwapo. Imechukua miaka 50 kwa Tanzania Bara kumuenzi Abdul Sykes na mdogo wake Ally na kuwapa medali katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru. Hii ndiyo historia ya nchi yetu Tanzania na Afrika kwa ujumla."
    [1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
    Like · Reply · 1 min · EditedUkitaka 

  • Ukitaka habari zaidi ingia hapo chini:
  • http://www.mohammedsaid.com/2013/12/dk-vedasto-kyaruzi-daktari.html

No comments: