

Nouru ya Ramadhani
Nouru
ya Ramadhani ni kipindi ambacho kimeweza kudumu kwa kipindi cha miaka 5 na
maudhui yake makubwa ni kuwaelimisha waumini masuala mbalimbali ya kifiqhi,
tarekhe, tafsiri n.k.
Kipindi
cha Nouru ya Ramadhani kimekuwa maarufu kwa wakazi wa Unguja na kuanzia mwaka
jana kutokana na kungana na Radio Nouru na Hits FM kipindi hiki kimekuwa
kimevuka mipaka ya Unguja mjini na kuweza kusikika mashamba, Pemba na kufika
hadi Bagamoyo.
Kipindi
hiki hurushwa kila siku ya Ramadhani kuanzia Saa 4 ya usiku hadi 5 na nusu
usiku. Kipindi huendeshwa kwa mtindo ambao umekuwa kivutio kwa watizamaji na
wasikilizaji, anakuwa muongozaji ambaye huwauliza masuala Masheikhe au Ustadh
wawili, muongozaji huuliza masula juu ya mada Fulani, mfano ilipofika tarahe 17
Ramadhani mada ilikuwa Vita vya Badr, muongozaji alitaka kujua kilichopelekea kupiganwa
kwa vita, maandalizi ya vita, vita vyenyewe, ushinda namna ulivyopatikana na
funzo kwa Waislamu wa zama hizi. Masuala baina ya muongozaji na Masheikh
huwenda kwa saa na nusu ikisha saa na nusu “line” huwekwa wazi na watazamaji pamoja
na wasikilizaji hupata fursa na wao kuuliza masuala na kujibiwa.
Uwanja
huu wa Nouru ya Ramadhani hushiriki Masheikhe ambao takriban wote ni wasomi
waliomaliza Vyuo vikuu mbalimbali ikiwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Chuo Kikuu cha
Makka na Madinah, Sudan, Libya, Yemen n.k
Waongazi
wa vipindi wakiwa wanapishana kwa kila kipindi cha siku mbili ni Ustadh Hamza
Z. Rijal (Ben Rijal) ambae kwasasa ni mwenye kuandikia gazeti la An-Nuur
akiandika makala juu ya wasomi wa Kiislamu waliopita na masuala ya Mazingira
katika Qur’an, aidha kuna Sheikh Mohammed Sleiman Hibry huyu ni mratibu wa
Radio Nouru aidha kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 anaandika Tahariri na
kuisoma katika Radio Zanzibar- ZBZC na sauti yake imezoeleka kuisoma tafsiri ya
Qur’an katika Channel mbalimbali kama Asalam, TV Africa n.k. Aidha kuna
mtangazaji maarufu wa ZBC TV na Radio Ndugu
Hafidh Kassim hushiriki katika waongozaji.
No comments:
Post a Comment