Quote By ushiboy View Post
USTIN MORRIS A-40

-Gari aina ya- Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari hilo kwa vijana wa TANU kwa kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
Ushiboy,
Hili gari Mwalimu Nyerere alipewa na Dossa Aziz.
Napenda nikuwekeeni hapa historia ya gari hili:

''...Dossa Aziz alipokwenda Nairobi mwaka wa 1946 alimkuta Ally Sykes, kijana maarufu na mwenye shughuli zake pale mjini akijulikana na takriban kila mtu. Dossa Aziz alikuwa amekwenda Nairobi kufanya usaili wa mafunzo ya urubani. Kulikuwa na vijana wawili kutoka Tanganyika, wote watoto wa matajiri. Dossa Aziz alikuwa katika usaili na mtoto wa Mwarabu mmoja tajiri, Ally Mmanga. Dossa Azizalikataliwa kufanyiwa usaili kwa kuwa alikuwa Mwafrika.

Waingereza walidai kuwa Waafrika hawakuwa tayari kufundishwa urubani. Dossa Aziz alifadhaika sana. Alimpigia simu baba yake huku akilia na kumpasha habari hizo. Ili kumliwaza mwanae, baba yake Dossa, Aziz Ally, alimtumia fedha anunue gari kama kifuta machozi. Gari hili lilikuja kuwa ndiyo chombo cha kwanza cha usafiri kwa TAA, TANU na Julius Nyerere.

Ally alimpeleka Dossa Aziz kwenye mkutano wa KAU ambao Kenyatta ilikuwa ahutubie. Wajaluo wakiwa kabila hasimu na maadui wa Wakikuyu, kabila ya Kenyatta, walikuwa wakipita huku na kule katika mkutano ule wakimtukana Kenyatta. Jambo hili lilianzisha mapigano kati ya Wajaluo na Wakikuyu. Mapigano yalifuatia pande zote mbili zikitupiana mawe. Askari wa kuzuia fujo wakiongozwa na maafisa wa Kizungu waliitwa kutuliza fujo. Waliizingira River Road, mahali ambapo mkutano ulikuwa ukifanyika na wakaanza kushambulia kwa virungu Mwafrika yoyote waliyemwona.

Dossa Aziz alishuhudia mambo haya yote kwa mshangao mkubwa. Baada ya kununulia gari, Dossa Aziz alikaa na Ally siku chache kisha akarudi nyumbani. Alirudi Dar es Salaam na kumbukumbu zile alizozishuhudia pale River Road, mjini Nairobi.''