Masahihisho kidogo katika hotuba ya mwalimu kuhusu siku za awali za tanu
Katika hotuba hii ya Mwalimu Nyerere kuna jambo kakosea. Anasema safari ya kwanza kutangaza TANU alikwenda Mbeya. Hapana safari ya kwanza alikwenda Morogoro akiongozana na Zuberi Mtemvu 1954 na hii safari ya Mbeya aisemayo alozungumza na wanachama mkutano wa ndani ilikuwa mwaka 1955 alipokwenda Lindi akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani. Mbeya TANU ilikuja baadae sana. Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utayakuta haya na ithibati yake ni nyaraka nilizosoma katika majalada ya akina Sykes.
''Nyerere
na msafara wake ulipokelewa na uongozi wa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji
kidogo nje ya mji. Msafara wa Nyerere ulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa
moja jioni hivi na giza lilikuwa linaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale
wajumbe wawili waliokutana na Nyerere mjini Dar es Salaam mwezi uliopita,
hakuna hata mtu kati ya umma ule uliokuja kupokea ujumbe kutoka makao makuu ya
TANU aliyekuwa anajua Nyerere anafanana vipi. Mpunga, dereva wa lori,
alijibagua kutoka kwa lile kundi la watu akawa amesimama pembeni ili Nyerere
apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtia Mpunga
machoni, Mpunga alimwendea kumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha
aliligeukia lile kundi la watu kumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja
jina lake kwa sauti kubwa. Baada ya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere.
Nyerere na ujumbe wake ulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya
TANU kwenye nyumba ya Mnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuwepo nyumba ya
seremala mmoja, Issa bin Ali Naliwanda. Hii ndiyo nyumba iliyochaguliwa alale
Nyerere na ujumbe wake, si kwa sababu ilikuwa nzuri kupita zote. Ilichaguliwa
na kupewa heshima hii kwa sababu ilikuwa karibu sana na ofisi ya TANU na hivyo
basi ilirahisishia TANU kazi ya ulinzi wa Nyerere. Siku iliyofuata ilikuwa
Jumapili na Nyerere aliwaomba wenyeji wake apelekwe kanisani kwa ajili ya
ibada.
Kanisa
Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya
Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna
mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye
viwanja vya kanisa. Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa
Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi
katika ofisi za serikali. Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa
miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa
Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika
uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala
hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala
mahali popote pale. Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo
yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala
hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa
Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize
Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.
Jumapili
hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na
walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa
hii ‘’maalum’’ ilidumu katika fikra za
wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo
liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii
huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku
akiwa amesimamiwa na Waislam.
Huenda mkutano aliokusudia Mwalimu Nyerere kuufanya Mbeya ni huu aliofanya Mkindani nyumbani kwa Ahmed Adam baada ya kutoka Lindi:
''Julius
Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi
siku ya Jumamosi. Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote
waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza
Nyerere. Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo,
aliyemiliki nyumba moja ya fahari. Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na
ilijengwa kwa mawe na chokaa. Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na
ujumbe wake. Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka
yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza. Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi
aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani. Huenda alichukuliwa Misri mwishoni
mwa mwa karne ya kumi na tisa na
Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani wakati wa
vita vya Maji Maji. Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya
Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo. Katika Vita Kuu ya
Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza. Baada ya
vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita,
Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya
Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe. Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee
iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa
kuhusudika.
''Kasella
Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii
ilikuwa mwaka wa 1952.Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa
wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa
miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi,
kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ‘’kuandika’’
ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia.
Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ngíambo uhamishoni na hata baada ya
kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya
mawili ya kihistoria, kuwa ''aliandika,'' katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa
TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika
harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.
Uongozi wa TAA haukurasimu katiba mpya.
Katiba ya TANU ilinukuliwa neno kwa neno kutoka Convention Peopleís Party (CPP)
ya Kwame Nkrumah, kwa kutia TANU mahali pa CPP. (Maelezo kutoka kwa Tewa Said Tewa).''
Kuhusu kutoa jina la TANU:
''Ilikuwa ni pale Anfal ambapo, huku vita vinafikia ukingoni, Abdulwahid na askari wenzake wa Burma walikaa kitako kutafakari mambo yaliyowasibu katika vita na kuufikiria mustakbal wa Tanganyika. Iliamuliwa kuwa askari wa Burma kutoka Tanganyika waliokuwa batalioni ya sita wawe ndio chanzo cha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuuhamasisha umma. Wote waliafiki wazo hilo. Jina lililochaguliwa kukitambulisha chama hicho lilikuwa Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes anamkumbuka Abdulwahid kiliandika jina la chama hicho kilichokusudiwa ndani ya shajara yake. Hawa askari wa Burma walikuwa wakifahamu vyema kuwa tayari huko nyumbani kulikuwapo na African Association, chama ambacho kilikuwa kikipigania haki za Waafrika. Abdulwahid alitarajiwa afahamu hili zaidi ya wenzake kwa sababu baba yake ndiye aliyekianzisha chama hicho akiwa katibu wake wa kwanza. Lakini suala la jinsi wangelivyokiunganisha chama hicho kipya cha TANU na kile cha African Association ili kudai uhuru, halikujadiliwa.

Kuhusu kutoa jina la TANU:
''Ilikuwa ni pale Anfal ambapo, huku vita vinafikia ukingoni, Abdulwahid na askari wenzake wa Burma walikaa kitako kutafakari mambo yaliyowasibu katika vita na kuufikiria mustakbal wa Tanganyika. Iliamuliwa kuwa askari wa Burma kutoka Tanganyika waliokuwa batalioni ya sita wawe ndio chanzo cha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuuhamasisha umma. Wote waliafiki wazo hilo. Jina lililochaguliwa kukitambulisha chama hicho lilikuwa Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes anamkumbuka Abdulwahid kiliandika jina la chama hicho kilichokusudiwa ndani ya shajara yake. Hawa askari wa Burma walikuwa wakifahamu vyema kuwa tayari huko nyumbani kulikuwapo na African Association, chama ambacho kilikuwa kikipigania haki za Waafrika. Abdulwahid alitarajiwa afahamu hili zaidi ya wenzake kwa sababu baba yake ndiye aliyekianzisha chama hicho akiwa katibu wake wa kwanza. Lakini suala la jinsi wangelivyokiunganisha chama hicho kipya cha TANU na kile cha African Association ili kudai uhuru, halikujadiliwa.
Abdulwahid
alilitumikia jeshi nchini Kenya, Ceylon, India na Burma. Hata kabla hajafikisha umri wa miaka ishirini
na mmoja alikuwa amekwishapanda cheo na kufikia Regimental Sergeant Major. Hiki
kilikuwa ndio cheo cha juu kabisa ambacho Mwafrika aliruhusiwa kukifikia. Cheo
kingine cha juu ambacho kiliwekewa Mwafrika kilikuwa kile cha Kapteni ambacho
Waingereza walimtunukia Kabaka Edward Mutesa wa Buganda na Chifu Adam Sapi
Mkwawa wa Wahehe. Lakini Kabaka Mutesa na Chifu Adama Sapi Mkwawa walitunukiwa vyeo hivi kwa sababu ya nyadhifa
zao kama machifu, wakati Abdulwahid alizipata tepe zake kwa sababu ya ujasiri
wake, kipaji chake cha uongozi na umaridadi wake. Vilevile Abdulwahid alivishwa
nishani kadhaa, baadhi yake Burma Star na ile ya War Medal.
![]() |
Kushoto: Ahmed Rashad Ali, Abdallah Jabir na Balozi Hemed Uwanja wa Ndege 1998 |
Baada
ya Vita Vya Pili kumalizika, Wazungu waliruhusiwa kuondoka uwanja wa mapambano
kurudi makwao kabla ya Waafrika, huku ikidaiwa kuwa wao walikuwa wakihitajika
haraka sana huko Ulaya kwa ajili ya ujenzi wa nchi zao zilizoteketea kwa ajili
ya vita. Vikosi vya Waafrika vilipewa ruhusa mwisho. Askari wa KAR kutoka
Tanganyika walikusanywa katika kambi moja iliyokuwa ikijulikana kama Kalieni,
nje ya Bombay, kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani. Walipokuwa Kalieni
Abdulwahid alikutana na rafiki yake toka nyumbani, Ahmed Rashad Ali,
Mzanzibari. Ahmed Rashad alikuwa mcheza kandanda mashuhuri na alikwenda India
kwa masomo. Tutakutana na Ahmed Rashad hapo baadaye tutakapojadilia harakati za
kudai uhuru huko Zanzibar. Askari kutoka Tanganyika walikuwa na maroli ya juu
walipokuwa baharini wakirudi nyumbani; kitu pekee kilichotawala mazungumzo yao
kilikuwa ni jinsi wangevyoweza kuwaondoa Waingereza kutoka ardhi ya Tanganyika.''
![]() |
Nakala ya kwanza ya kitabu cha Abdul Sykes kwa Kiingereza kilichochapwa London mwaka wa 1998 maelezo hayo hapo juu yanatoka katika kitabu hiki |

Waasisi wa TANU mbele ya Makao Makuu ya TAA New Street 7 July 1954
Nyuma waliosimama aliyevaa miwani ya jua ni Abdulwahid Kleist Sykes
Ilipokuwa ofisi ya TAA na TANU sasa lipo jengo hili jipya la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba Avenue |
No comments:
Post a Comment