Aman Thani |
Aman Thani ni mmoja wa wapigania uhuru wa Zanzibar na alipata kuwa Secretary General wa Zanzibar Nationalist Party mwaka wa 1963 akishika nafasi ya Abdulrahman Babu baada ya Babu kujitoa chama na kuunda chama chake Umma Party. Aliwekwa jela Zanzibar na Tanganyika baada ya mapinduzi. Aman Thani ni kati ya wanasiasa wachache waliobaki katika kundi lile lililopigania uhuru wa Zanzibar. Ameandika kitabu mashuhuri kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ''Ukweli ni Huu.''
Kauli ya CCM Zanzibar jana kuwa Zanzibar si ya machotara bali ni ya Waafrika imekurupusha sege la nyuki wakali. CCM imekuwa ikilaniwa na kila mtu kote duniani khasa kutoka kwa wafuatiliaji wa siasa za Tanzania hususan visiwani Zanzibar.
Msome Aman Thani akieleza dhana ya Uafrika katika siasa za Zanzibar:
‘’...huenda ikawa tukakosana juu ya hili neno, ‘’Muafrika.’’ Kwangu mimi, ‘’Muafrika,’’ ni yoyote aliyezaliwa na
kuishi katika kontineti la Afrika. Si muhimu asli ya kabila lake wala rangi ya
mwili wake. Hapana shaka kuwa huu ndio msimamo wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika.
Basi sijui kwa wengine Muafrika ni wa namna gani? Suruti awe wa rangi nyeusi na
nywele za pilipili? Akiwa mweupe na nyele ndefu za singa, na wazazi wake wote
wawili wamezaliwa Zanzibar, huyo hakubaliwi kuwa ni Muafrika?’’
''Maelfu kwa maelfu ya
roho za wananchi wa Congo, Burundi na Rwanda kila uchao zinapotea kwa sababu ya tafauti za
ukabila. Roho zilizopotea Zanzibar kwa ujinga kama huu wa ukabila si kidogo
ukilinganisha na udogo wa nchi yake. Bado ndugu zetu wamo katika kutaka kuzidi kuzipepelea kuni za fitina ya ukabila. Inshaallah
Wazanzibari wa leo hawataumwa tena na
nyoka mara ya pili katika pango lilelile moja. Wameshakuwa makini wanawatambua
waliokuwa wema wao na waliokuwa waovu wao, yaliopita wameyaweka visogoni mwao.''
''Sisi Waisilamu badala ya kukamatana kama tulivyoamurishwa na dini yetu, tunameguana kwa kufuwata propaganda za maadui wanazotujengea kukhusu rangi, asli na ngozi zetu za mwili. Inasikitisha kuwa sumu hii bado mpaka hivi sasa imo ndani ya nyoyo za baadhi ya ndugu zetu.''
''Sisi Waisilamu badala ya kukamatana kama tulivyoamurishwa na dini yetu, tunameguana kwa kufuwata propaganda za maadui wanazotujengea kukhusu rangi, asli na ngozi zetu za mwili. Inasikitisha kuwa sumu hii bado mpaka hivi sasa imo ndani ya nyoyo za baadhi ya ndugu zetu.''
No comments:
Post a Comment