TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: HUJUMA ZA BARAZA LA MITIHANI DHIDI YA WAISLAM
Kila sifa njema anastahiki Allah,
ambaye rehema zake zimeenea katika kila kitu katika ulimwengu bila ya kujali
utii ama uasi wa kitu hicho katika amri na sharia zake.
Rehema na amani zimuendee kipenzi
chetu mtume Muhammad (S.A.W) kwa kuwa kiigizo chema na rehema kwa walimwengu
wote.
Ndugu waandishi kwa muda mrefu
waislam wamekuwa wakiilalamikia suala zima la utendaji wa serikali kuwa umekuwa
wakibaguzi kwa kuwapendelea wakirsto kwa kuwapa nafasi mbalimbali muhimu
serikalini na katika taasisi zake.
Ndugu waandishi na Waislam mnamo
tarehe 01/ 05/2012 Baraza la mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya kidato
cha Sita, matokeo hayo yaliwashtua sana wanafunzi waislam waliofanya mtihani wa
elimu ya dini ya kiislam (Islamic Knowledge). Takriban asilimia 70 walifeli kwa
kupata daraja F, na asilimia 30 ndio waliofaulu tu.
Katika hao waliofaulu walipata alama za juu kabisa nchi
nzima ni wanafunzi saba tu ambao wamepata daraja D, kwa matokeo haya somo hili
likawa somo la mwisho kwa ufaulu nchi nzima (rejea kitabu cha takwimu cha
Baraza la mitihani Tanzania April 2012.
Matokeo haya yaliwashtua wazazi
na walimu wa somo hili, baadhi ya
wanafunzi waliamua kukata rufaa ya kutokubaliana na matokeo hayo.
Waislam kupitia Taasisi mbali
mbali za kiislam walimuandikia katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi kumuomba aunde tume huru kuchunguza matokeo ya somo husika.
Kufuatia malalamiko hayo ya
baadhi ya taasisi za dini, baraza la mitihani liliyatazama matokeo hayo na
kugundua pia walikosea na hivyo Baraza la mitihani likaidhinisha kutolewa
matokeo mapya kwa somo hilo.
Mabadiliko hayo ya matokeo ufaulu
kwa wanafunzi wale wale ambao awali walifeli kwa asilimia 70, sasa yakabadilika
na ufaulu ukaongezeka kwa zaidi ya asilimia 70.
Kwa namna yoyote ile itakavyokuwa
dosari kubwa kama hii ni kashfa kubwa
kwa Baraza la mitihani Tanzania na Serikali kwa ujumla.
Na kwa kutilia maanani muundo na
historia ya utendaji wa wa baraza la mitihani la Tanzania kama nilivyoanza
kuelezea, Waisla wanayokila sababu ya kuamini
kwamba matokeo haya ni
uthibitisho tosha wa hujuma ambazo wanafunzi wa kiislam walikuwa wakifanyiwa
kwa muda mrefu.
Na hii inatupa picha kwamba
dosari hizi zilizotokea kwenye somo la maarifa ya kiislam, haziishii kwenye
somo hili, bali uchunguzi ukifanyika kwa masomo yote waliofanya wanafunzi wa
kiislam itadhihirika kwamba hila na dhulma kama hizi zinafanyika katika masomo
mengine.
Kimsingi kwa dhulma hii
waliyoifanya baraza la mitihani dhini ya wanafunzi wa kiislam, Bakwata na
waislam wote kwa ujumla wamepoteza imani na baraza la mitihani la Tanzania na
hasa katibu mtendaji wake .
Bakwata, linawapongeza na
kuwaunga mkono Taasisi zote za kiislam nchini kwa jitihada ya kuligundua hili
na hatua walizozichukuwa dhidi ya baraza la mitihani na kuhufahamisha umma wa
kiislam juu ya kadhia hii.
Sheikh Ponda Issa Ponda akiomba dua kabla ya kuanza kwa maandamano dhidi ya NECTA |
Tunarudia baraza tunawapongeza
taasisi zote za kiislam na tunasema katika hili Bakwata tuko nyuma yao kwani
kauli yao ndio kauli yetu.
Bakwata, inamshangaa Katibu
mtendaji wa Baraza la mitihani (Necta) Dk. Joyce Ndalichako, kwa kauli yake
aliyoitoa kupitia vyombo mbali mbali vya habari vya jana tarehe 5/06/2012,
akisema hakuna hujuma na mitihani inasahihishwa na walimu wenye
sifa,wanachaguliwa na na wakuu wa shule zao, walimu wenye uzoofu na kuna mfumo
wa usahihishaji aliohuita “Conveyor Belt”.
Bakwata inasema hapa tatizo la
msingi sio mitihani kusahihishwa na walimu wenye sifa,na nani anawachagua
walimu hao wenye sifa au huo mfumo wa
usahihishaji, tatizo la msingi
hapa ni kufelishwa kwa makusudi kwa wanafunzi wetu wa kiislam katika somo
husika, wakati nakala za mitihani yao (Scripts) zinaonyesha wamefaulu.
Bakwata, tunahoji kwanini tatizo
hili la huo mfumo (Conveyor Belt) litokee mwaka huu, mbona matokeo ya mwaka
jana waislam hawakulalamika na kulikuwa hakuna dosari kama za mwaka huu iweje
itokee mwaka huu, wakati mfumo ni ule ule?
Bakwata, tunaamini waislam katika
hili tumehujumiwa na waislam hawajaridhishwa na majibu ya Dk. Ndalichako, aliyoyatoa kupitia vyombo vya
habari vya hapa nchini.
Hiyo mifumo ya usahihishaji sio
maneno matakatifu kwamba haiwezi kuchezewa kutokana hila za binadamu ni mifumo
iliyowekwa na binadamu, na binadamu huyohuyo anaweza kuibadilishabadilisha
vyovyote anavyotaka.
Sisi kama Bakwata,tunaamini ili
kurudisha imani ya waislam dhidi ya Baraza la mitihani tunataka mambo yafuatayo
yafanyike,
·
Tume
huru iundwe la kuchunguza Baraza la mitihani la Tanzania na utendaji wake wa
kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
·
Katibu
mkuu wa baraza la mitihani (Necta) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya jamuhuri
ya muungano wa Tanzania na Baraza la Mitihani.
·
Watendaji
wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa kompyuta ya Baraza la
mitihani nao wawajibishwe mara moja.
·
Hatua
za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa baraza la mitihani
watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.
·
Muundo
wa baraza la mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama
hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea baraza la mitihani sura ya
kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha makatibu wakuu watendaji na manaibu katibu
wakuu wamekuwa wakristo na wenyevyiti wa baraza hilo ni wakristo tangu
lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.
·
Pia
tunaiyomba Serikali iwape nafasi wanafunzi wote ambao baada ya matokeo yao
kubadilishwa wamekuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu waruhusiwe kuomba
mikopo bodi ya mikopo, tunalisema hili kutokana na muda
wa kuomba mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kwisha.
Suala la Sensa ya watu na makazi.
Kama tunavyojua kwa mwaka huu wa
2012, kuna zoezi la sense ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika
kuanzia mwezi wa nane, 2012, na kutoka na upotoshaji ulioenea kwenye vyombo vya
habari hapa nchini, kalenda iliyochapichwa na ofisi ya waziri mkuu, imetoa
takwimu zinazoonyesha idadi ya watanzania ni milioni 43 ambapo kwa mujibu wa
dini zao wakristo ni asilimia 52, waislam asilimia 32 na dini zingine ni
asilimia 16.
Bakwata tunalaani kitendo hiki na
tunasema takwimu hizi sio sahihi na zinapotosha wananchi, hii ni kwa sababu
katika sense zilizofanyika hivi karibuni ikiwemo sense ya mwaka 2002 kipengele
kinachobainisha dini za watanzania kiliondolewa.
Kwakuwa taarifa hizi zinaonekana
kwenye kalenda zinazoonyesha zimetayarishwa na ofisi ya waziri mkuu, tunaitaka
serikali kurudisha kipengele kinachobainisha dini za watanzania katika sense ya
mwaka huu ili ukweli ujulikane na kuondoa kabisa sintofahamu hii.
SUALA LA MGOGORO WA HIVI
KARIBUNI ZANZIBAR
Ndugu waandishi wa habri naamini
nyinyi nyote kama waandishi wa habari mnajua au mmesikia vurugu zilizohusisha
imani za dini zilizotokea visiwani humo na kutokana na taarifa nyingi za
vyombao vya habari zilizokuwa zikitolewa tangu mgogogro huu uanze kuna kila
dalili za kuchukuliwa hatua za haraka haraka na katika mazingira haya wale wote
waliohusika na vurugu hizi wasijulikane tena na watu wasio na hatia
wakahusishwa na hali ikawa mbaya zaidi kwa hivy o kutokana na kadhia yote hiyo
na yote yaliyosemwa na makundi mbalimbali ya waisla na wasiokuwa waislam Sisi
kama Bakwata tunasema yafuatayo:
Kwanza tunalaani kitendo cha
uvunjifu wa amani uliotokea Zanzibar na tunaamini waliofanya vurugu zote zile
sio waislam bali ni wahuni tu.
Pili tunasema Wazanzibar,
wasikilizwe kwa yale ambayo wanayapigia kelele kama malalamiko yao yapo katika
muungano Serikali haina budi kuyasikiliza
yale yote yanayolalamikiwa na
kuyarekebisha, kwani Muungano sio qur- an useme kilichomo humo hakiwezi
kurekebishika.
Tatu iundwe tume huru yenye
wajumbe kutoka pande zote, makanisa, Serikali na UAMSHO ili zichunguzwe tuhuma
hizi kwa undani zaidi maana kwa kweli athari zinaweza zikawa za muda mrefu
kwani zinapandikiza kutoaminiana baina ya Wazanzibar hasa wakristo na waislam
jambo ambalo halikuwepo hapo kabla na yoyote takae bainika kuwa na hatia sheria
ichukue mkondo wake bila ya kujali wadhifa alionao katika chama, dini ama
Serikali.
Mwisho tunamuomba Allah atupe
Imani ya kweli katika nchi yetu na kama kuna fisadi na adui Allah amdhalilishe
hapahapa Duniani, amen.
Wabillah Tawfiq.
Sheikh Issah Bin Shaabani
Simba.
Sheikh Mkuu na Muft wa Tanzania
No comments:
Post a Comment