Tuesday, 19 January 2016

KUTOKA FACEBOOK: ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE 1955

Mwl.Julius K. Nyerere akikabidhiwa meza ya ofisi yake ya TANU na wazee wa DSM! Mmoja ya walio ktk picha hii ndiyo alitengeneza meza hiyo.Je tunawajua wazee hawa?Na hapo ni wapi ktk DSM hii?Karibuni kwa michango yenu wana D'salaam.
Comments
Ramadhani Matimbwa Mungu awarehemu Wazee wetu hawa kwa kazi kubwa walizozifanya ktk harakati za kuikomboa nchi hii.Japo leo hawatajiki lakini Mwenyezi Mungu atawalipa inshallah! Tunashuhudia leo watu wananeemeka ktk CHAMA chetu bila jasho!
Nurdin Khamis Tujitahidi tuliobaki tushirikiane kuenzi wazee wetu kama Saigon sport club kila mwaka kwa dua mji umevamiwa tutashuhudia meya wajiji mkuria au mchaga aibu
Sule Mavitu wazee hao mola awalaze mahala pema
Mohamed Said Hizo samani zilitengenezwa na Bwana Ali Msham aliyekuwa na kiwanda chake Mtaa wa Kariakoo. Alifika ofisini kwa Nyerere New Street Makao Makuu ya TANU akamkuta Nyerere anafanya kazi katika meza ambayo Ali Mshama aliona haina hadhi ya rais wa TANU. Ndipo alipoamua kumtengenezea Nyerere samani mpya zitakazoendana na heshima yake na heshima ya TANU. Hii ilikuwa mwaka wa 1955. Wakati huo Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu hapo Magomeni Mapipa. Hapo kwenye tawi la TANU nyumbani kwake ndipo ilipopigwa hiyo picha siku alipokaribishwa Nyerere kuja kupokea samani kwa ajili ya ofisi yake. Pamoja na samani Nyerere alipewa na saa ya ukutani na vitu vingine.Hawa wazee wengi wametangulia mbele ya haki. kwa hakika walikuwa wazalendo wa kweli na walijitolea hali na mali kupambana na ukoloni. Ali Msham ni huyo aliyesimama wa kwanza kulia na aliyekaa kwenye meza ni Julius Nyerere.

No comments: