Wednesday, 20 January 2016

KUTOKA FB: MJADALA WA ALI MSHAM NA JULIUS NYERERE

  1. Allen KilewellaVerified User 

    #4
    Yesterday at 10:04 PM
    Joined: Sep 30, 2011
    Messages: 1,114
     
    Likes Received: 113
     
    Trophy Points: 63



    Picha nzuri na inaonesha jinsi Mwalimu alivyokuwa hana hila wala kudharau wengine hata kwa michango yao midogo waliyotoa. Viongozi waliofuata baada yake utu wao anaujua Mungu pekee!!
    SIGNATURE


  2. M

    Mohamed SaidVerified User 

    #5
    Yesterday at 10:22 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 7,053
     
    Likes Received: 93
     
    Trophy Points: 48






    Allen,
    Huo haukuwa mchango mdogo.
    Ulikuwa mchango mkubwa sana.

    Achilia mbali thamani ya samani.
    Wakati ule kujinasibisha na TANU ilikuwa kujitafutia matatizo na wakoloni.

    Ali Msham alijitolea chumba kimoja nyumbani kwake kiwe ofisi ya TANU.
    Hakuishia hapo alimfungulia Mama Maria Nyerere kijiduka kidogo cha
    kuuza mafuta ya taa.

    Jioni nyakati za Maghrib ishaingia mtoto wa Ali Msham alikuwa ndiye
    akimsindikiza Mama Maria nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.

    Wakati ule Magomeni miembe mitupu na kiza kikiingia panatisha kwa
    mwanamke kutembea peke yake.
    1. Mo

      SexerJF-Expert Member

      1. #36
        Today at 1:12 PM
        Joined: Oct 22, 2014
        Messages: 1,273
         
        Likes Received: 28
         
        Trophy Points: 48
        New




        kwa hiyo wewe unataka na diallo atajwe kwa kuwa tu alimsaidia magufuli kuingia ikulu?!
        SIGNATURE

      2. Troojan

      TroojanJF-Expert Member

      1. #37
        55 minutes ago
        Joined: Oct 8, 2012
        Messages: 391
         
        Likes Received: 14
         
        Trophy Points: 18
        New




        Yaaan ni shidaa aiseee.
      2. Mumba Daly

      Mumba DalyJF-Expert Member

      1. #38
        47 minutes ago
        Joined: Jun 13, 2014
        Messages: 799
         
        Likes Received: 82
         
        Trophy Points: 28
        New




        Hujui kitu,subiri ugali ukiiva huitwe ukale
      2. Andrew Nyerere

      Andrew NyerereVerified User 

      1. #39
        43 minutes ago
        Joined: Nov 10, 2008
        Messages: 2,288
         
        Likes Received: 44
         
        Trophy Points: 48
        New


        Mama Maria hakuwa na duka kwa Ali Mshamu au popote
      2. Sexer

      SexerJF-Expert Member

      1. #40
        32 minutes ago
        Joined: Oct 22, 2014
        Messages: 1,273
         
        Likes Received: 28
         
        Trophy Points: 48
        New




        mkuu, kwa hiyo tumedanganywa!
        SIGNATURE

      2. Mumba Daly

      Mumba DalyJF-Expert Member

      1. #41
        24 minutes ago
        Joined: Jun 13, 2014
        Messages: 799
         
        Likes Received: 82
         
        Trophy Points: 28
        New




        Si rahisi wewe kupendezwa na simulizi kama hiyo,wewe hufurahishwa na ile kama siyo juhudi zake nyerere uhuru tungeupataje?
      2. M

      Mohamed SaidVerified User 

      1. #42
        3 minutes ago
        Joined: Nov 2, 2008
        Messages: 7,054
         
        Likes Received: 94
         
        Trophy Points: 48
        New




        Sexer,
        Mimi sina sababu ya kusema uongo.

        Historia ya TANU ni maarufu kwa wazee wengi wa Dar es Salaam ya 1950 ambao wakati ule
        walikuwa vijana wengine katika Bantu Group 1955 kabla haijawa TANU Youth League 1958.

        Mama Maria alikuwa pia na duka la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikikichi jirani na nyumba ya
        Mwalimu Fatina.

        Kama ninavyopenda kusema siku zote si lazima uamini historia hii.

        Kuwa wewe umesoma haya niliyoandika na ukakutana na haya ya akina Ali Msham ambayo
        kabla ya leo hukuwa umeyasoma popote au kuyafahamu kwangu mimi inatosha sana.


    2. Trojaan,
      Nimekusoma na nimeona kuwa huijui historia ya mapambano dhidi ya dhulma za wakoloni.

      Historia hii ni moja wala haigawanyika kati ya akina Abdulrauf Songea Mbano na Selemani Mamba majemadari wa Vita Vya Maji Maji waliotoa roho zao 1905 - 1907 na hawa akina Ali Msham waliotoa fedha zao kupambana na ukoloni.

      Hawa walikuwa wakipokezana kijiti.
      Hebu soma hii:

      ALI SONGEA MBANO
      JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI

      Suleiman Mamba

    3. Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

      Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

      Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

      Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

      Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

      Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

      “Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

      Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

      Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:
      Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

      Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

      Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

      Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

    4. Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale. Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah. Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao.


    5. Ilunga Hassan Kapungu
      Jumanne 19 Oktoba 2010




No comments: