''Hakuna
nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha
mpango wa kushughulikia hali ya siasa.
Kuelewa mwelekeo wa siasa kama wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo
wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti
yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza alilofanya Abdulwahid mara tu
baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo
ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha yeye
mwenyewe Abdulwahid, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika; Dr.
Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya
Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni
kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo
hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati
za kudai uhuru wa Mtanganyika.''
Kutoka kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''
No comments:
Post a Comment