Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad na Sheikh Ahmed Islam |
''Mwaka
a 1986, miaka miwili kabla, baada ya takriban miaka ishirini na tano ya ukimya,
Ally Sykes alikubali kufanya majadiliano na mwandishi wa Kiingereza kutoka Africa Events, Paula Park.
Park akachapisha majadiliano aliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes na mchango wao katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa
marafiki zake na kwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale
yaliyoandikwa katika gazeti lile kweli yeye ameyasema. Haukupita muda mrefu,
maofisa wa Idara ya Uhamiaji walimtembelea Park na kumuomba aondoke nchini.''
Kutoka kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''
Baraza la Wazee wa TANU 1955 |
No comments:
Post a Comment