Monday, 8 February 2016

ALI MSHAM, TAWI LA TANU NA DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA NYERERE






UncleBen,
Simama kwenye ukweli.
Penye ukweli uongo hujitenga.

Tuanze na historia ya Ali Msham.

Ali Msham alikuwako na picha zake na tawi la TANU aliloanzisha nyumbani
kwake wanae wamenipa na mimi nikaziweka katika mtandao.

[​IMG]
Kulia wa kwanza Ali Msham aliyekaa kwenye meza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Sote tumeziona.

Picha zile zimemuonyesha Ali Msham akiwa na Nyerere, John Rupia, Zuberi
Mtemvu, Sheikh Suleiman Takadiri, Bi. Titi Mohamed 
na wazalendo wengine
miaka ya 1954/55.

Mtoto wa Ali Msham, Abdulrahman Ali Msham ndiye alionieleza mimi historia ya
baba yake wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.

Kuhusu duka la mafuta ya taa wanasema baba yao alimuanzishia Mama Nyerere
mradi wa kuuza mafuta ya taa na kabla ya kufungua duka wakiuza katika kwama.

Baadae biashara ilipokua ndipo Ali Msham akamfungulia Mama Maria duka pale
nyumbani kwake.

Abdulrahman alinieleza kuwa Mama Maria katika kazi alizokuwa akifanya pale
dukani alikuwa akifuma sweta na alikuwa na kijana wake Joseph Kiboko Nyerere.

Kijana aliyekuwa akimsindikiza Mama Maria jioni kurejea kwake alikuwa Abdallah
Omari Likonda
 ambae alikuwa mpwa wake Ali Masham.

Huyu Abdallah Omari Likonda yu hai hadi leo.
Ikiwa leo hii historia hawaitaki wala hapana haja ya ubishi.

Historia ya TANU iliandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni College mwaka wa 1981.
Jina la Abdulwahid Sykes halikutajwa popote lakini mimi nimeandika kitabu kizima
kuhusu mchango wake katika TAA na TANU.

Mimi nawaachia wasomaji wangu waamue wenyewe nani mkweli na nani muongo.

[​IMG]
Abdulrahman Ali Mshama akiwa amesimama nje ya nyumba yao ilipokuwa tawi la TANU 1954/55

No comments: