Tuesday, 2 February 2016

GAZETI LA UHURU NA HABARI LEO NA MARUDIO YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR KATIKA JF


singidadodoma said: 
[​IMG][
/QUOTE]
SingidaDodoma,
Jambo moja ambalo lazima lizingatiwe katika post hii ni kuwa hao BAKWATA hawakubaliki kwa
Waislam.

Nimeanza na kauli hii kwa sababu kinachoonekana kuvutia ni kuwa BAKWATA wametoa kauli
kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na wanavyochukulia gazeti la Uhuru ni kuwa ikiwa BAKWATA
wametoa sauti basi wanawasemea Waislam.

Ieleweke kuwa huyo Alhad Mussa inasemekana ni mwanachama wa CCM kwa ajili hiyo basi
haishangazi kwa yeye kuja na kauli hiyo.

[​IMG]

Wala hapa sina haja ya kusema kuwa na huko BAKWATA Alhadi Mussa ni sheikh wa BAKWATA
wa mkoa si sheikh wa BAKWATA wa nchi nzima.

Ukweli ni kuwa BAKWATA haikubaliki na Waislam wengi toka ilipoanzishwa mwaka wa 1968.
Unaweza kupata historia yote ya BAKWATA hapo chini:
Mohamed Said: BREAKING NEWS/HEART BREAKING NEWS: KIBARAKA BAKWATA YAUNGA MKONO KURUDIWA UCHAGUZI ZANZIBAR

 singidadodoma said: 
[​IMG][/

QUOTE]
SingidaDodoma,
Vyama hivyo washiriki uchaguzi gani ndugu yangu ilahili katika uchaguzi uliopita hawakuweza
hata kupata 1% ya kura?

Si ndiyo tuanazidi kujifedhehesha kwa dunia na kuonekana kioja?
Uchaguzi umefanywa na umemalizika salama.

CCM Zanzibar wawe waungwana wakubali kushindwa wasubiri uchaguzi
ujao.

No comments: