Hata alipokuwa CCM na mimi mwandishi wa habari
tumefanya kazi ya kiungwana kujali maisha ya watu kwa mfano kipindi cha mauaji
2001...pia wakati wa mzingiro wa Mtendeni.... tulikutana kubishana juu ya
mitizamo yetu pale kwake Migombani.
Haigopi kutoa mawazo yake na
haigopi kukosolewa na mwenye dira, kisima cha ujuzi na taarifa kiasi wengine
wanamwita mjuaji.
Nikakutana nae mara kadhaa
tukielekea uchaguzini na unaona wazi juu ya sio uwazi na udhati lakini uthabiti
katika anachokiamini kwa mfano kuwa Dk. Shein
hakushinda 2010 na ndio maana akazama kwenye MUWAFAKA na ndio chanzo kikubwa
cha kuwa adui.
Sisikitiki kuwa leo yupo sero wala sitalia akienda
gerezani kwa sababu hakuna gereza la kumuweka mtu mwenye moyo mkubwa kama Eddy
Riyami.
Ni dalili za mwisho za kumalizika
utawala ambao ulikataliwa Oktoba 25...
Naamini Eddy
Al Mugheiry hajuti,
haguni wala halii maana anajua tupo nae na tutasimama nae.
FREE EDDY RIYAMI
No comments:
Post a Comment