
Unahitaji kukutana na Eddy
Riamy mara moja, siku moja na takriban mkazungumza kwa kiasi cha dakika tano
na atabaki kichwani kwako. Hakuna sehemu utayaoingia katika historia na siasa
za Zanzibar ikawa yeye ni mwanafunzi. Allah amemjalia kuitumikia nchi yake
Zanzibar vilivyo katika uzalendo wa hali ya juu kabisa toka akiwa kijana mdogo
sana. Siku nilipokutananae kwa mara ya kwanza alinishangaza jinsi alivyokuwa anaijua
historia ya Bara na wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika
historia ambazo zinagusa pande zote mbili za muungano. Alinishangaza sana jinsi
anavyoweza kuunganisha matukio katika siasa za Visiwani na Bara kisha akafanya
na utabiri ambao kwa mara nyingi inapotokea mimi huiambia nafsi yangu kuwa Eddy
alipatapo kunigusia jambo hili.
Eddy Riamy ni bingwa
wa ‘’Facts and Figures,’’ hili niligundua siku mmoja tumekaa pamoja wakati wa
uchaguzi uliopita nyakati za jioni kama kawaida kila tukikutana mazungumzo yetu
ni maendeleo ya nchi yetu na nini kifanyike kujenga utengamano katika jamii.
Aliyonieleza siku ile ndiyo yaliyokujatokea kuwa CCM haitashinda uchaguzi Zanzibar.
Eddy akanipa na ‘’indicators,’’ yaani viashiria. Mimi nilimgusia ‘’Gerrymandering,’’
iliyokuwa imepitika Zanzibar yaani ukataji mpya wa majimbo ya uchaguzi. Jibu
alonipa lilinishangaza sana. Eddy alinambia haitosaidia kubadilisha ‘’pattern’’
ya upigaji kura. Lazima nikiri kuwa wakati mwingine ilibidi nijikunyate kama
mwanafunzi makini anaetaka kulijua somo ili apasi mtihani wa profesa wake. Kwa
nini nilikuwa wakati mwingine nakaa kimya kwa sababu nilikuwa kwa kweli sielewi
ile mantiki ya ushindi katika ‘’Gerrymandering,’’ ya Zanzibar. Kilichionifanya
mimi nifunge mdomo wangu ni kuwa nilikuwa najua nazungumza na mjuzi.
Nakumbuka alipatapo siku
moja kunambia kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ndiyo dira
itakayowaongoza Wazanzibari katika neema. Alinieleza mengi kuhusu juhudi
zilizopitika hadi kufikia pale na vipi ‘’referendum’’ ilivyofikiwa na vipi
Wazanzibari kwa mara ya kwanza walipeleka ujumbe ulio wazi kwa viongozi wao nini
walichokuwa wanakitaka na kutegemea kutoka kwao. Eddy ‘’Master of Figures’’
pale pale akaniuliza, ‘’Hivi unajua kwa Wazanzibari kupiga kura 66.7% kutoka
SUK wewe unajua maana yake?’’ Nimetumbua macho namsikiliza mwalimu wangu
ananisomesha. ''Hii itakuja kujiakisi katika hata upigaji kura kwenye uchaguzi
mkuu unaokuja,'' Eddy aliniambia. Naweza kusema mengi sana kuhusu Eddy Riyami. Eddy ni mzalendo wa
kweli na Eddy ni mtu shujaa na mwenye akili pevu na uwezo mkubwa sana wa
kusimamia kile anachokiamini.
Eddy si mtu wa kuificha
sura yake na kutoa matusi kuwatukana viongozi wa nchi. Vitu kama hivyo vya
kujificha uso vinafanywa na watu waoga. Eddy hana sababu ya kutoa matusi. Huo
uwanja wa matusi unao wenyewe. Huo si uwanja wa Eddy. Viwanja vya Eddy hakuna
Mzanzibari asiyevijua. Eddy kasimama saa saba mchana na kufanya aliyofanya kwa
wazi kila mtu akishuhudia. Eddy hawezi kujifungia chumbani akamwaga matusi
kwenye ''digital recorder'' kisha akairusha hewani.
Naamini katika dhati ya moyo wangu kuwa
hakuna kitu kitachoma moyo wa Eddy kama ile kudhaniwa ati yeye ni mtoa matusi.
No comments:
Post a Comment