Monday, 1 February 2016

MJADALA WA UCHAGUZI WA ZANZIBAR KATIKA JF

jingalaoJF-Expert Member

#35
Today at 7:50 PM
Joined: Oct 12, 2011
Messages: 6,330
 
Likes Received: 198
 
Trophy Points: 63
Mkuu hebu kuwa muungwana...mada yako inahusu ubaguzi ni mada nzuri sana...lakini umeingiza ushabiki kwa kusema ccm Zanzibar haijashinda ...sielewi umetumia utafiti gani na kama ni sahihi kutumia utafiti kutangaza kuwa ccm haijashinda...labda ungesema kwa mujibu wa CUF ...CCM haijashinda nisingekutaka ufute hiyo kauli.

kuna muda tuweke ushabiki pembeni...hata mimi siwezi kusema mshindi kwa kuwa mwenye mamlaka hayo hajatangaza mshindi!!

Hata huku bara wafuasi wa UKAWA wanaamini wameshinda lakini NEC ndiye aliyetutangazia mshindi.

Nakushauri ufute hiko kipengele halafu turejee kwenye mjadala wa ubaguzi kulingana na ushahidi' ulioleta

***

 Jingalao,
Mwaka wa 2011 nilishiriki katika kipindi cha Meza ya Duara kinachoendeshwa na 
Sauti ya Ujerumani.

Washiriki wengine wenzangu walikuwa Salehe Feruzi wa CCM Zanzibar, Ahmed Rajab (London), 
Dr. Harith Ghassany (Washington DC) na mimi nikizungumza kutoka Tanga.

Mwenyekiti alikuwa Othman Miraj kutoka Bonn aliyetuunganisha kwa simu.

Nilimwambia Salehe Feruzi hayo niliyoeleza hapa kuwa CCM Zanzibar hawajapatapo kushinda
uchaguzi.

Bwana Feruzi akaniomba ushahidi kama unavyoniomba wewe hii leo.
Nikamwambia kuwa inasikitisha kuwa yeye kiongozi wa juu wa CCM Zanzibar lakini hajui hilo.

Nikamuongozea kitu kingine.

Nikamwambia kuwa CCM Zanzibar wanaogopa uchaguzi na nikamweleza yale wanayofanya
kuwazuia wafuasi wa CUF kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Baada ya haya ndipo nikamkumbusha barua ya Ali Ameir katika uchaguzi wa mwaka wa 1995
baada ya CCM kushindwa waliyakataa matokeo.

Haya yote niliyosema hapa ni kweli wala si ushabiki.
Tujadili haya kabla hatujakwenda mbele katika chaguzi zilizofuatia.

***
Nilikuuliza swali kuhusu kuitwa mchochezi hujalijibu!
Nimekueleza kuwa mamlaka ya kumtaja mshindi wa Zanzibar ni nani hujaongekea hilo....ukikamatwa kwa uchochezi utakuwa umeonewa?

Mimi sikulazimishi wewe kusema kuwa CUF imeshinda ...lakini ninachohoji ni nani aliyethibitisha hilo?

Ili mada yako ya ubaguzi ijadiliwe kwa muktadha wa uwazi na ukweli na bila kujali itikadi ni vyema ukaondoa huo msimamo wa CCM kushindwa Zanzibar kwa kuwa hatuna matokeo ya uchaguzi hadi sasa...unapoendelea kuwa mshabiki wa msimamo huo unatoa fursa kwa mwanaccm au yoyote ambaye ni mchangiaji huru kuchukua upande kwenye swala hili ambalo naliona ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Unategemea mwanaccm anayepinga ubaguzi achangie kwa uhuru ilhali umeshaweka msimamo wako kisiasa??

Kama lengo lako ni kujadili ubaguzi bila kujali itikadi za kisiasa huna budi kufuta kipengele cha CCM HAIJASHINDA ZANZIBAR...ni rahisi sana kama kweli wewe ni msomi...

CCM kuogopa uchaguzi Zanzibar haimaanishi kuwa wanashindwa katika uchaguzi!!

Futa hiko kipengele au badilisha na kusema kwa mujibu wa CUF au kwa mujibu wako tujue msimamo wako!!

Tambua kwamba hata mimi nina nasaba na undugu huko Zanzibar na Oman pia!

***

Jingalao,
Niwie radhi kuhusu ''uchochezi.''
Nilijibu swali hilo katika bandiko langu huko nyuma.

Inaelekea limekupita.
Itapendeza ukiwa unasoma na post za nyuma hii itakusaidia kutojirudia.

Jibu langu liko hapo chini:
Kizibao,
Tunaweza tukajadiliana kwa heshima ikiwa tutatumia lugha za staha.
Ukianza mjadala kwa lugha za ''pia,'' hatutofika mbali.

Nakushukuru kwa kunifahamisha kuwa kuna ''Machotara Hizbu,'' na
''Machotara,'' wengineo.

Hili sikupata kulijua kabla.
Hayo mengine ulosema sina ujuzi kwa hiyo nitawaachie wengine wachangie.

Kuhusu uchochezi nitashukuru kunifahamisha wapi nimechochea.
Kwa kumalizia ningependa uingie hapa yapo mengine:
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016

Jingalao,
Vipi tena unakuja na mambo ya kukamatwa kwani wewe unahusika na vyombo
vya sheria?

Hili swali la kumtangaza mshindi mbona Maalim Seif kalieleza kwa kirefu kuwa
yeye hakutangaza ila yale matokeo yalokuwa yameshatolewa.

Fanya rejea katika mkutano wake na waandishi wa habari utakuta taarifa zote.

Sina haja ya mie kurudia barua ya Ali Ameir aliyekataa matokeo baada ya CCM
kushindwa kwenye uchaguzi wa 1995.

Hebu ingia hapa kuna mengi utajifunza:
Mohamed Said: NAMDURUSU ALI AMEIR UCHAGUZI WA ZANZIBAR 1995 NA JABIR IDRISSA

Sina cha kufuta kwani haya niandikayo nimeyafanyia utafiti na najua ukweli wake.

***

Ndio maana nikasema urekebishe hoja yako pale juu iwapo unafanya reference za ki-CUF.

Kurekebisha haitakucost chochote zaidi ya kuiweka hoja yako huru!..au weka reference yako kuwa 'nimemsikiliza maalim Seif akijitangaza mshindi'

Ondoa hiyo itikadi tujadili hoja kwa uhuru!

***

Jingalao,
Nimejitahidi kukueleza na si lazima ukubaliane na mimi.
Ninapoingia JF mimi silengi kuzungumza na mtu mmoja.

Huingia humu kuzungumza na umma kwa kile Allah kwa
hisani yake alichonijaalia.

Naamini wengi wamenufaika.

***

Hata mimi ninapoingia JF Siingii kuzungumza na mtu mmoja bali naingia kuzungumza na wengi wenye uelewa mdogo na mkubwa...kama nilivyojaliwa na mwana wa Mungu yesu kristu!!

Na kwa jina la Yesu maelezo yangu hueleweka kwa wengi ukiacha maruhani wachache!

HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SIO KILIO AU VIHOJA!

***

Jingalao,
Ahsante kwa fikra zako.

***

Sihitaji shukrani mkuu nahitaji majibu ya hoja!

***

Jingalao,
Nifahamishe jibu lipi utakalo kutoka kwangu.
Shukurani ni katika adabu za mazungumzo.

No comments: