Salim Msoma |
Utangulizi
Hapo chini ni barua niliyopokea kutoka kwa Salim Msoma akitia maoni kuhusu makala, ''Uchaguzi wa Zanzibar wa Mwaka wa 1961,'' ambamo niliweka nukuu ya Aman Thani akieleza uchaguzi uli ulivyokuwa.
Wasiomfamahu Salim Msoma ni kuwa Msoma ni katika wasomi makini wa wakati wa mapinduzi ya Afrika. Alikuwa mwanachama wa University Students's African Revolutionary Front (USARF) chama ambacho kilianzishwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka wa 1967 na wanachama wake walikuja kuacha alama katika historia za ukombozi wa nchi zao kama John Garang na Yoweri Musevani.
Wasiomfamahu Salim Msoma ni kuwa Msoma ni katika wasomi makini wa wakati wa mapinduzi ya Afrika. Alikuwa mwanachama wa University Students's African Revolutionary Front (USARF) chama ambacho kilianzishwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka wa 1967 na wanachama wake walikuja kuacha alama katika historia za ukombozi wa nchi zao kama John Garang na Yoweri Musevani.
Sheikh Mohamed Said,
Ahsante kwa kutuletea maandishi
haya ambayo yanatukumbusha historia ya karibuni ya Zanzibar.Bila shaka waraka
huu umeunakili kutoka kijitabu alokiandika mzee wetu Bw Amani Thani Fairuz
miaka kadha iliyopita na ambacho binafsi nilibahatika kukisoma.Mimi naomba
nitoe maoni ya mawili matatu kuhusu maelezo ya Mzee Amani Thani.
Kwanza nakubaliana nawe kuwa yapo ya
kujifunza katika kadhia ya uchaguzi wa Januari na June 1961 Zanzibar khasa
tukitilia maanani hali ya kisiasa ilivyo hii leo visiwani.Lakini ninalotaka kuchangia
mimi ni kwamba maelezo ya Mzee Fairuz kama yalivyo maandishi mengine kuhusu
mada hii niliyoyasoma yanakuwa na upungufu mmoja. Nao ni tabia ya kuelezea
matukio (facts) bila ya kujadili kwa upana na kutafsiri yaliyo nyuma ya matukio
hayo yaani muktadha wake. (broad discussion of related issues surrounding the
narrated events).Kwa mfano unapozungumzia suala la kuwepo VITI katika majimbo
ya uchaguzi vilivyokuwa vinagombewa na kueleza matokeo ya chama kile kilipata
viti kadhaa na kingine kikapata viti zaidi na kushinda bila ya pia kuonyesha
TAKWIMU za kura zilizopigwa hakutowi picha sahihi kwa wasomaji kuhusu mfumo
mzima wa chaguzi zile. Hivi leo waandishi mbalimbali wanaeleza na kuonyesha
jinsi ukataji wa majimbo (constituencies) ulivyokuwa wa mashaka na hila. Imebainika
majimbo yaliyokuwa na wafuasi wengi wa ASP yalitengewa viti vichache wakati
majimbo yalokuwa na watu kidogo wa ZNP yalipewa viti vingi. Ujanja huu ambao
Waingereza wanauwita 'gerrymandering' ndio hatimae uliwapokonya ushindi halali
ASP na kutulea mabalaa na maafa visiwani. Wasomaji lazima waelimishwe kuwa
miongoni mwa sababu za kufanyika Mapinduzi Zanzibar ni hili la kunyimwa kwa
hila na ujanja haki yao ASP ya kuunda na kuongoza serikali.
Jengine ninalotaka kulieleza kwa mnasaba
huu huu wa kujadili mambo badala ya kuyataja tu kijuu juu ni kitendo cha Sheikh
Mohamedd Shamte kujitoa ASP mwaka 1960. Bw Fairuz ameeleza haelewi sababu za
Mzee Shamte kujitoa ASP. Lakini kadri ya muda ulivyopita imebainika wazi kuwa
ZPPP kilikuwa ni chama kilichotokana na tawi lililokuwa la Shirazi Association
huko Pemba. Mara zote imekuwa ikitolewa picha potofu kuwa Waswahili wa Zanzibar
waliojitambulisha kwa jina la Shirazi Association walikuwa ni kitu kimoja (homogeneous).
Kumbe hali ni tofauti kabisa. Washirazi wa Pemba na hata baadhi ya wale wa
Unguza wamekuwa wakati wakiwemo ndani ya chama cha ASP wakipinga kile
walichokihisi ujenzi wa uhusiano wa karibu kati ya ASP na TANU. Shamte
aliwakilisha hisia hizo na alikuwa hamuamini kabisa Julius Kambarage Nyerere
kinyume na alivyokuwa Mzee Karume. Na Mzee Shamte alipohisi huu usuhuba wa
Nyerere na Karume unazidi kushamiri ndipo akagombana na Mzee Karume na kuamua
kujitoa ASP. Lakini kuna jambo jengine ambalo ZNP hawakupenda kuliongea. Nalo
ni kwamba huyu Mzee Shamte hapo mwanzoni alikuwa hawaamini pia Waarabu!
Inaelezwa kuwa katika mwaka ule (1959) ambao Mzee Karume kwa shinikizo la
PAFMECA alianza kuhutubia mikutano kupitia jukwaa moja na Sheikh Ali Muhsin,
Shamte alikuwa ni ‘’diehard,’’ mmoja wapo aliekasirishwa ndani ya ASP. Cha
kustaajabisha ni kumuona mtu yule yule alokuwa akipinga kumuona Karume akiwa
pamoja na Ali Muhsin alikuja baadae kuunda Umoja na huyohuyo Ali Muhsin kuanzia
uchaguzi wa 1961 na hatimae akapewa Uwaziri Mkuu ndani ya Serikali ya Uhuru
1963! Haya ndio mambo ambayo waandishi kama Bw Fairuz wanapaswa kuyasema kwa
uwazi zaidi. Wasalam.
No comments:
Post a Comment