''Aman Thani ni ukurasa katika kurasa tukufu za kitabu cha Zanzibar''
Mohamed Ghassany
Aman Thani (1927 - 2016) |
Historia za Afrika zimegubikwa na historia rasmi. Historia ya uhuru wa Zanzibar haikusalimika. Historia ya Zanzibar inaanza na kumalizika kwenye mapinduzi ya mwaka 1964. Historia ya uhuru wa Zanzibar inapoelezwa na atakapotajwa Amani Abedi Karume picha itakayojengwa ni ile ya kueleza jinsi Afro-Shirazi Party ilivyokuwa ikihangaika kuwakomboa ‘’wakwezi’’ kutoka makucha ya Hizbu. Hutosikia harakati za kupigania uhuru na juhudi zilizopita za viongozi wengine kama Ali Muhsin akiongoza Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kuikomboa Zanzibar kutoka ukoloni wa Mwingereza.
Nilipigiwa simu usiku
muda mwingi na mtayarishaji wa kipindi
Maalum cha Mapinduzi Day akanitaka radhi na kuniomba kama nitaweza kufika Azam
TV ili nishiriki katika kipindi cha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Nilikubali na hapo hapo nikaningia maktaba kuangalia nini ninaweza kusema siku
ya pili katika kipindi kile. Hapo ndipo iliponijia fikra kuwa nitaongeza
ufahamu wa watu wengi khasa vijana wa kizazi hiki cha sasa kama nitamueleza
Aman Thani hata kwa mukhtsari kama mmoja wa wazalendo waliopigania uhuru wa Zanzibar.
Nilianza kutalii nyaraka za Aman Thani na kutuma picha Azam TV ili zitayarishwe
kwa kipindi tunachotarajia kukifanya siku ya pili mapema asubuhi kwenye kipindi
maarufu ‘’Morning Trumpet.’’
Waliokuwa Zanzibar wanatazama Azam TV asubuhi ile waliiona picha yake kwenye televisheni kwa mara ya kwaza katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 na wakasikia historia yake.
Waliokuwa Zanzibar wanatazama Azam TV asubuhi ile waliiona picha yake kwenye televisheni kwa mara ya kwaza katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 na wakasikia historia yake.
No comments:
Post a Comment