Aman Thani |
(Aman Thani kutoka kitabu chake kipya
ambacho hakijachapwa)
Hayo hapo juu ni kutoka
katika kalamu ya Aman Thani akiandika katika kitabu chake cha pili (hakijachapwa).
Hakika ni
maneno mazito na yenye kufikirisha.
Aman Thani amefariki leo
alfajir Dubai ambako alikimbilia kiasi cha miaka 40 iliyopita baada ya kutoka
jela alikofungwa Tanzania Bara. Aman Thani ameacha hazina kubwa ya kumbukumbu
zake binafsi kuhusu vipi hali ikuwa wakati wa kupigania uhuru na wakati baada ya
mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 ambayo yeye kila alipozungumza aliyaita ‘’mavamizi.’’
Aman Thani ameandika vitabu viwili. Kitabu chake cha kwanza, ‘’Ukweli ni
Huu’’ kitabu ambacho kama jina lake lilivyo Aman Thani alirekebisha mengi
katika propaganda ambazo kwa hakika zimevuruga historia ya Zanzibar. Kitabu hiki kilichapwa mwaka wa 1995. Kitabu cha
pili alikikabidhi kwa ajili ya uchapaji na kipo katika ngazi ya uhariri.
Namshukuru Allah kuwa nillibahatika kukutana na Aman Thani Dubai mwaka wa 1999 nilipomtembelea nyumbani kwake Rashidiya na alinikabidhi nakala kadhaa za kitabu chake ''Ukweli ni Huu,'' akanambia niwape wenzangu wengine wasome wajue ukweli.
Katika blog hii majuma
machache yaliyopita nimeweweka video tisa za Aman Thani mwenyewe akizungumza kuhusu
historia ya Mapinduzi ya Zanzibar. Video hizi zimevutia watazamaji wengi kiasi
inaniwia shida kwa sasa na kwa hakika sina maneno yanayoweza kutosha kumueleza
yeye na yale aliyoshuhudia na kutenda katika kupigania uhuru wa Zanzibar. Laiti
Aman Thani asingetuachia hazina hii mengi ambayo sasa yamekuwa hadhir kwetu
yangepotea. Nawaachia wasomaji wamsikilize Aman Thani mwenyewe akiirudisha
hadhira yake nyuma miaka 50 iliyopita kuujua ukweli katika historia ya
Zanzibar.
Tafadhali msikilize marehemu Aman Thani akieleza yale yaliyopitika Zanzibar baada ya mapinduzi:
No comments:
Post a Comment