ACT HAITASHIRIKI UCHAGUZI WA ZANZIBAR, WAMTAKA MAGUFULI ASIKWEPE MAJUKUMU
Kiongozi wa chama cha ACT wazalendo ndugu Zitto amesema chama anacho kiongoza hakitashiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar kwa kile alichokisema kuwa ZEC haina mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi.
Katika kuweka msisitizo amemtaka rais Magufuli kuingilia mkwamo uliopo Zanzibar, ACT haiamini kuwa mgogoro wa kisiasa Zanzibar utamalizwa kisheria sababu badala yake ina amini utamalizwa kisiasa, na kwa sababu hiyo ni lazima rais wa Muungano aingilie.
ACT imeshutushwa na kauli ya rais kutaka wenye malalamiko juu ya ZEC waende mahakamani ikiwa ni hivi juzi tu serikali imetoa fedha kwa mahakama sharti la mahakama kushughulikia kesi ambazo zitaiingizia serikali fedha, ushawishi wa serikali kwa mahakama unatoa taswira halisi juu hukumu ya kesi itakayofunguliwa zidi ya ZEC.
Zubeir Zitto Kabwe na Mwandishi |
No comments:
Post a Comment