Monday, 28 March 2016

KUTOKA JF: MJADALA WA HAMAD RASHID

Utangulizi
Wafalme wa Ulaya wa enzi zilizopita walikuwa katika majlis zao wanakuwa na watu wakijulikana kama ''court jesters,'' 

Hawa kazi yao ilikuwa kuchekesha pale alipo mfalme kwa nia ya kumchekesha mfalme mwenyewe na waliomzunguka. 

Hawa Court Jesters hadi leo wapo katika karne hii ya 21 na wanafanya kazi ile ile ya uchekeshaji. 

Mfalme na yeye katika kuwaadhimisha hawa wachekeshaji anapopata fursa ya kuwazungumza huwasifia mwisho wa kusifia.

Mathalan tumesikia Zanzibar kumetoka vyama ambavyo vitagombea nafasi ya urais kupambana na Dr. Shein.

Hawa wagombea urais ndiyo ''Court Jesters,'' wa hizi enzi zetu wanafanya kazi ya kumfurahisha mfalme kwani bila wao Dr. Shein angejihisi upweke na unyonge kugombea nafasi ile muhimu ya urais wa Zanzibar akiwa hana mpinzani.

Kichekesho cha hawa  Modern Court Jesters kinakuja pale anapokabiliwa na kamera za televisheni.
Hapo ndipo patamu...

Anawaaminisha wananchi kuwa yeye anaingia katika uchaguzi kuishinda CCM Zanzibar na atakuwa rais mpya wa Zanzibar.

Mchekeshaji ni mchekeshaji na atabaki kuwa mchekeshaji.

Waandishi wa habari kukataa kuwa ''spoil sports,'' hawamuulizi, '' Ee bwana we nyie si ndiyo uchaguzi wa kweli 2015 jumla yenu mlipata kura 1%?

Hamuulizi kwa kuwa wanajua anachekesha watu bure bila ya kutoza kiingilio.


Hamad Rashid akitoka kupiga kura ya marudio





Kilasi Mkuu,
Sifa mojawapo anayotakiwa kuwanayo ''political scientist'' ni kuwa
na uwezo wa kutabiri yaani kufanya, ''prediction.''

Lakini utabiri huu si wa kupiga ramli ni wa kutazama hali ya hewa
kisha ukasema kwa hali hii niionayo na nikichukukia mambo fulani
hii inaweza ikawa hivi.

Mathalan unaweza kuangalia ushindi wa Dr. Shein ukasema sidhani
kama Tanzania atakujatokea rais akapata ushindi wa kishindo kama
wa Dr. Shein.
Unaweza hata ukashawishika kusema kuwa Dr. Shein anaweza akaingia 
Guiness Book of Records kwa ushindi ule.

Hamad Rashid yeye katika uchaguzi ule wa kweli wa 2015 vyama vyote 
vya upinzani kwa pamoja ukitoa CUF walipata kura jumla 1%

Hii nini maana yake?
Maana yake ni kuwa hamna kitu.

Hamna kitu kwa vipi?
Hamna kitu kwa sababu 1 iko karibu sana na 0.

Labda utaniuliza kwa nini isiwe karibu na 2?
Jibu ni kuwa safari ya mbele ni ngumu nyepesi ni ya kurejea nyuma.

Sasa hata kweli kuwa CCM hawajali sheria na hata kama kweli wanataka
kumpa umakamu wowote ule Hamad Rashid si lazima awe na kianzio?

Mtaji wa 3% kiasi ni shida.

Vipi Dr. Shein aliyevunja ''all time record'' ya historia ya chaguzi zote za
Zanzibar kuanzia ukoloni akiwa na ushindi wa 91.4% avunje heshima yake 
kwa kuhusishwa na mtu aliyevunja ''all time record'' ya kushindwa kwa 
kuwa na 3% ya kura?

Naona niishie hapa.

No comments: