Saturday, 26 March 2016

TAKWIMU ZA USHINDI WA DK. SHEIN NI ''FAIRY TALE'' HADITHI ZA KUWALAZA WATOTO USINGIZI - MOHAMED GHASSANY

Utangulizi
Wakati nasoma shule ya msingi Dar es Salaam ya 1960s moja vitu tukipenda kusoma ni ''fairy tale,'' hizi ni hadithi za kitoto zilizokuwa zikitutoa dunia hii na kutupeleka dunia nyingine ya kufikirika. 

Wakati ule nilikuwa mtoto wa kiasi cha miaka 12. Hadithi hizi zikija katika vitabu tukiita, ''comics.'' Jina lenyewe linajieleza. 

Kulikuwa na  ''Jason and the Golden Fleece,'' ''Jack and the Beanstalk,''‘’Cinderella,’’ ''The Princess and the Frog,’’ na nyingine nyingi. 

Hadithi zote hizi zilikuwa ni visa ambavyo kuwezekana kwake kutokea ilikuwa labda kwa sababu ya miujiza lakini kwa hali ya kawaida isingewezekana katu. 

KIla nisomapo mambo ya Zanzibar kazi hizi ''classics,'' katika fasihi mashuhuri za dunia hunijia. Mikasa Zanzibar haimaliziki ni sawa na ule usemi kuwa ‘’Kwa kungwi hakwishi nyimbo.’’ 

Hiki ndicho nilichokiona wakati napitia hizi takwimu za uchaguzi wa Zanzibar wa Marudio. 

Wapiga kura hawakuonekana vituoni kiasi wasimamizi wanalalia meza kuchapa usingizi lakini matokeo yanaonyesha wapiga kura walifurika vituoni. 

Hakika chochote kinawezekana katika siasa za Zanzibar wala usibishe.

Hebu soma nyambulizi hizi hapo chini kutoka Kalamu ya Ghassany ambae yeye kakiita kisa hiki ''Miujiza ya Busu la Jecha Lililomgeuza Chura Kuwa Mwana Mfalme,'' kisa kilichopo kwenye ''The Princess and the Frog,’’ 

Mohamed Said

''Tafauti ya kura kwa kila jimbo imeandikwa kwa wino mwekundu na kuwekewa alama ya + kumaanisha kuwa ni ongezeko lililozidi kwenye kura ya 20 Machi.

Ongezeko la kura za Dk. Shein kisiwani Unguja

Na.
JIMBO
OKT. 2015
MACHI 2016
TAFAUTI
1.
CHWAKA
6,067
8,294
+2,227
2.
UZINI
9,941
12,995
+3,054
3.
DIMANI
4,818
7,122
+2,304
4.
PANGAWE
3,009
5,168
+2,159
5.
MTONI
5,336
7,977
+2,641
6.
TUNGUU
7,589
10,589
+3,000
7.
CHUMBUNI
4,892
8,954
+4,062
8.
KIWENGWA
2,995
3,539
+544
9.
MAHONDA
4,352
5,665
+1,313
10.
NUNGWI
3,556
4,064
+508
11.
MPENDAE
3,974
6,642
+2,668
12.
MFENESINI
4,192
5,790
+1,598
13.
KIJINI
2,396
2,787
+391
14.
MAGOMENI
5,445
8,173
+2,728
15.
MTOPEPO
3,671
6,788
+3,117
16.
M/KWEREKWE
4,003
9,597
+5,594
17.
MWERA
2,554
3,449
+895
18.
BUBUBU
4,356
6,593
+2,237
19.
CHAANI
4,120
5,208
+1,088
20.
PAJE
5,585
7,099
+1,514
21.
WELEZO
2,528
4,033
+1,505
22.
BUMBWINI
2,351
3,490
+1,139
23.
JANG’OMBE
6,216
8,810
+2,594
24.
KIKWAJUNI
5,998
9,942
+3,944
25.
CHUKWANI
3,571
5,922
+2,351
26.
MKWAJUNI
4,285
4,351
+66
27.
MAKUNDUCHI
8,161
9,800
+1,639
28.
FUONI
889
1,386
+497
29.
K/SAMAKI
4,413
6,976
+2,563
30.
MALINDI
2,334
5,873
+3,539
31.
KWAHANI
5,960
9,360
+3,400
32.
DONGE
5,255
5,308
+53
33.
TUMBATU
5,424
6,081
+657
34.
AMANI
4,107
6,026
+1,919
35.
KIJITOUPELE
4,373
6,911
+2,538
36
SHAURIMOYO
5,593
9,006
+3,413

Hapa tusifanye uchambuzi wala tusifanye majumuisho, bali tusome tu hizi nambari kwa kuzingatia tafauti iliyopo. Katika ongezeko hilo, unaweza kuona kuwa kwenye baadhi ya majimbo, siku ya tarehe 20 Machi, Dk. Shein alipigiwa kura na “watu” 3,000+ wa ziada kutoka wale wa 25 Oktoba. Hiyo ndiyo hadithi ya Uzini, Tunguu, Mtopepo, Kikwajuni, Kwahani na hata jimbo la Malindi ambalo ni ngome ya CUF.

Majimbo yaliyotia fora katika haya ni la Mwanakwerekwe, ambako watu 5,594 wa ziada walijitokeza ‘kumpigia’ kura Dk. Shein siku ya tarehe 20 Machi, ikilinganishwa na wale wa Oktoba 25. Jimbo hilo linafuatiwa na la Chumbuni, ambalo lina ongezeko la kura 4,062.

Jimbo pekee ambalo linaweza kusemwa kuwa na ongezeko dogo kabisa kwa kura za Dk. Shein katika haya 31, ni la Donge ambalo liliongeza 53 tu likifuatiwa na Mkwajuni ambalo lina kura 66 za ziada.

Kwa msingi huo, matokeo yaliyopo hapa yanalinganisha kura alizoambiwa amepata Dk. Shein katika uchaguzi wa Oktoba 25 na zile ambazo ZEC inasema alizipata tarehe 20 Machi kisiwani Pemba.

Na.
JIMBO
OKT. 2015
MACHI 2016
TAFAUTI
1.
CHAMBANI
725
3,129
+2,404
2.
MTAMBILE
798
3,093
+2,295
3.
KIWANI
1,499
3,892
+2,393
4.
MKOANI
3,110
6,407
+3,297
5.
CHAKECHAKE
1,113
4,551
+3,438
6.
CHONGA
1,515
3,598
+2,083
7.
OLE
617
3,818
+3,201
8.
WAWI
1,243
4,147
+2,904
9.
ZIWANI
571
2,890
+2,319
10.
GANDO
795
3,298
+2,503
11.
MTAMBWE
320
1,789
+1,469
12.
MGOGONI
637
3,395
+2,758
13.
KOJANI
1,003
3,994
+2,991
14.
WETE
863
3,737
+2,874
15.
KONDE
691
1,606
+915
16.
MICHEWENI
1,436
3,273
+1,837
17.
TUMBE
372
1,520
+1,148
18.
WINGWI
394
2,062
+1,668

Hapa napo unaona ongezeko kubwa lililopo kama ilivyokuwa kwa Unguja. Majimbo yaliyotia fora kwa ongezeko ni Chake Chake (3,438), Mkoani (3,297) na Ole (3,201), huku ziada ndogo kabisa ikiwa jimbo la Konde, ambapo Dk. Shein ameongeza kura 915, ikifuatiwa na jimbo jirani la Tumbe, ambako kuna ziada ya kura 1,148.

Matokeo haya ‘yamepatikana’ hata baada ya ripoti za waandishi wa habari na mashahidi waliokuwepo siku ya tarehe 20 Machi kote visiwani Unguja na Pemba kuelezea idadi ndogo kabisa ya wapiga kura vituoni, kufuatia CUF na vyama vyengine tisa kutangaza kuususia uchaguzi huo.

Matokeo haya ‘yamepatikana’ pia hata baada ya picha za mnato na za vidio kusambaa mitandaoni zikionesha namna baadhi ya wale waliojitokeza kupiga kura walivyozifanya kura hizo ndani ya vituo – kuchorachora kwa nia ya kuziharibu.

Lakini kama nilivyotangulia kusema, huu si uchambuzi wala tafsiri ya chochote kilichotokea, bali ni wasilisho tu la namna busu la kimiujiza la Bint Mfalme lilivyofanikiwa kumgeuza chura akawa Mwana Mfalme.''


No comments: