Friday, 25 March 2016

MUADHAMA POLYCARP PENGO NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA





Kwa kiasi cha juma zima hivi mitandao ya kijamii imeweka picha hiyo hapo juu ya Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhashama Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha imamuonyesha Kadinali Pengo akimfanyia maombi Bwana Makonda bila shaka akimuombea Mungu amuimarishe katika kazi yake mpya ili aifanye kwa ufanisi zaidi. 

Paul Makonda amepanda cheo kutoka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hadi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya Waislam wameonyesha hofu kubwa katika tukio hili na nadhani hofu hii imetokana na dhana ya Mfumokristo katika serikali ya nchi yetu. 

Binafsi nimeliangalia hili kwa jicho jingine kabisa nalo ni kuwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir keshafunguliwa njia na kiongozi mwenzake wa kiroho. 

Kadinali Pengo kadhihirisha kuwa vitu kama hivi vya kuwaita watendaji wa serikali ofisini na kuwaombea Mungu vinaruhusiwa. 

Mwito wangu kwa wale wenye hofu kuwa labda wataambiwa ''wanachanganya dini na siasa,'' ni kuwa waondokane na hofu hiyo na wasaidie kuwaondoa hofu viongozi wa Waislam ili na wao waige mfano wa Kanisa Katoliki.

Itapendeza siku moja kuona picha ya mtendaji Muislam yuko ofisini kwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir anasomewa Surat Yasin.

No comments: