Hiyo heshima aisemayo Mohamed Aboud kuwa ipo Zanzibar
heshima hiyo haipo.
Heshima ya Zanzibar imetoweka miaka mingi iliyopita.
Huwezi kuwa na uongozi wa sampuli iliyoko sasa madarakani
tena kwa kutumia mabavu nchi ikabaki na heshima yake.
Huwezi kuwa na wahuni wanatembea na silaha za jadi na za
kisasa mabarabarani wakipiga watu na kuvunja stesheni za
radio nchi pamoja na viongozi wake wakabaki na heshima.
Hebu tazama hii picha hapo chini chanzo chake ni gazeti la
Mwananchi la tarehe 22 Machi 2016.
Hii ni picha ya Mazombie.
Ikiwa msomaji anataka kuwajua zaidi hawa Mazombie na mfano wake
aingie Google atafute ''Ton Ton Macoute.''
Serikali yenye heshima haiwi na kikosi cha wahuni wanaopiga na kutesa
raia:
Heshima na utu wananchi anaozungumza Mohamed Aboud
uko wapi?
Au ndiyo hayo hapo juu?
Uhuru anaozungumza Mohamed Aboud uko wapi au ndiyo huu
hapo chini?
Zanzibar ilikuwa na heshima yake lakini hiyo heshima imepotea miaka mingi
sana.
Zanzibar ilishafikwa na shida ya njaa na wala sababu zake hazikuwa hizo
Mohamed Aboud anazozisema.
Hawa wanayofanya hii dhulma wakae wakijua.
Allah anashuhudia na ulimwengu unashuhudia.
No comments:
Post a Comment