TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
01 April 2016
CHINA MSIWE ADUI WA
DEMOKRASIA TANZANIA KWA MASLAHI YENU
Nchi ya China jana
kupitia balozi wake Dk.Lu Youqing alipokuwa anazungumza na waziri wa nchi ofisi
ya makamu wa Raisi Muungno na mazingira January Makamba alikaririwa na vyombo
vya habari akisema China inaamini uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Zanzibar ulikuwa
huru na haki.
Chama cha wanachi
CUF tunaelewa kwamba kwa nchi yeyeto inayofahamu Demokrasia,Uhuru na Haki ni
nini hawezi kuasema uchaguzi wa marudio Zanzibar ni wa huru na haki.Ama kama
nchi hiyo itaamini kwa haki na uhuru huo wa ZEC ya Jecha basi nchi hiyo
inamatatatizo sana ya Kidemokrasia nchini mwake.
CUF hatuamini kwamba
China haijui demokrasia ikoje ila wanahalalisha uchaguzi haramu wa Marudio
Zanzibar kwa sababu ya maslahi yao ya kiuchumi kwa raia wa China nchini
Tanzania na huko kwao China.
Chama kikongwe kinachotawala China CCP na kile chama tawala Tanzania CCM wamekuwa na uswahba wa muda mrefu.Uswahiba huu umefanya China kuwa kipofu kuhusu mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binnadamu na ukiukwaji wa demokrasia wakihofia kuharibu uswahiba wao na CCM.Uswahiba ambao unamaslahi zaidi kwa China kuliko Tanzania, ndio maana wako tayari kuhalalisha haramu kuwa halali.
Chama kikongwe kinachotawala China CCP na kile chama tawala Tanzania CCM wamekuwa na uswahba wa muda mrefu.Uswahiba huu umefanya China kuwa kipofu kuhusu mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binnadamu na ukiukwaji wa demokrasia wakihofia kuharibu uswahiba wao na CCM.Uswahiba ambao unamaslahi zaidi kwa China kuliko Tanzania, ndio maana wako tayari kuhalalisha haramu kuwa halali.
China inaamua kuungamkono kukandamizwa kwa demokrasia nchini Tanzania ili kujikomba kwa serikali ya CCM waendelee kupata hisani zaidi kwa masalhi ya taifa lao bila kujali CCM kwa kiasi gani inakuwa katili kwa watanzania.CUF Tumekuwa tukijaribu kuchunguza baadhi ya mambo ambayo yakihusisha wachina hapa nchini na kutilia shaka sana urafiki wa China wa Tanzania labda ni wakinafiki zaidi na kudalali maliasili za Watanzania.
China inapata tenda
kubwa za ujenzi nchini Tanzania mfano ujenzi wa barabara ambazo nyingine
zishaanza kuharibika,madaraja na majengo makubwa nchini.Hata mradi wa
kusafirisha gesi wamo pia.
Tanzania kumekuwa na ongezeko la wachina wakifanya biashara zainazofanywa na
watazania kama vile kuuza maua kariakoo,yeboyebo na sehemu mblimbali
nchini.Jambo hili limekuwa likitia wasiwasi sana hasa ukiuliza hawa ndio
wawekezaji waliokuja kuuza maua na yeboyebo.Swali hili serikali imekuwa
ikishikwa nakigugumizi namna ya kujibu.
Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya mauajia ya tembo .Changamoto
amabayo raia wa China wamekuwa wakishukiwa kuhusika.Mfano Novemba 2013 maeneo
ya Mikocheni Dar es Salaam,wachina watatu walikamatwa na vipande mia saba 700
vya meno ya tembo.
Tanzania inakabiliwa na chanagamoto ya bidhaa feki kutoka China.CUF tumekuwa
tukihoji ni kwa nini serikli imeshindwa kuzuia bidhaa hizi feki kutoka China a
mpaka leo hii bado zipo na zinaathiri uchumi. Chombo cha kudhibiti ubora wa
bidhaa nchi TBS kipo na bidhaa feki kutoka China zipo.
Raia kutoka China
wamekuwa wakiongezeka sana nchini na mara kadhaa baadhi yao wamekuwa
wakikamatwa kwa kuishi nchini bila kufuata utaratibu.
Chama cha wananchi CUF tunaionya sana China iache siasa kufumbia macho
ukiukwaji wa demokrasia nchini kwa maslahi yao na kuitumia Tanzania kujinufasha
na rasilimali zilizopo bila kujali amani itakapovunjika hapo baadae.Pia
tunaitaka serikali kw makini sana iangaliae mahusiano na misaada inayotolewa na
China inamalengo gani yaliyofichika kwa Taifa letu.
HAKI SAWA KWA WOTE
Mh.Abdalah Mtolea( MB)
Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF Taifa
0758811110
Mh.Abdalah Mtolea( MB)
Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF Taifa
0758811110
No comments:
Post a Comment