![]() |
| Nat King Cole |
Ahsante sana.
Niko hapa namsikiliza marehemu Abdul Haleem Hafidh
kupitia Sure Radio.
Huyu alikuwa mwimbaji mashuhuri Misri katika miaka
ya 1950.
Sasa wakati namsikiliza nikamkumbuka Dr. Dau.
Iko siku mimi na Dau tulikuwa Jeddah duka la CD.
Yeye akanunua CD za Abdulhalim Hakim.
Ikapita miaka siku moja mimi niko Muscat na Dr. Harith
Ghassany tuko duka la CD akaninunulia mimi CD za Nat
King Cole.
Dr. Ghassany akaniuliza nimchukulie na Dau zawadi ya Nat
King Cole.
Mimi nikamjibu nikasema, ''Sidhani kama Dau anamjua Nat
King Cole.''
Tukaangua kicheko.
Lakini Dau akipanda gari yangu kuna muziki wa Nat King Cole
alikuwa anasikia nikiuweka lakini hafatilii.
Basi akanunua CD za Abdul Halim Hafidh na Um Kulthum akanipa
nimletee.
Sasa nilipomfikisha Dau mzigo wake nikamwambia, ''Harith alitaka
kukununulia CD za Nat King Cole lakini mimi nikamwambia wewe
hujui hata huyo Nat King Cole ni nani?''
Tukaangua kicheko kingine.
Mwisho Dau akaniluliza mimi, ''Kwani Nat King Cole ananijua
mimi?''
Tukaangua kicheko kingine.
Ni miaka mingi sana sasa imepita.
Siku zile tulikuwa vijana sote mimi, Ramadhani na Harith.
Lakini mimi ni mzee na ni kaka yao.
Wenzangu bado vijana.
| Dr. Dau na Mwandishi Jeddah 1997 |
| Dr. Dau na Mwandishi 2014 |
| Dr, Harith Ghassany na Mwandishi Muscat 2015 |
| Dr. Harith Ghassany na Mwandishi Muscat 1999 |
| Dr Harith Ghassany na Dr Ramadhani Dau |
.jpg)
No comments:
Post a Comment