Huyo Bi. Mkubwa ni Mama Daisy.
Huyu mimi ni mama yangu.
Kushoto: Mama Daisy, mbele ni Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni Bi. Zainab mkewe Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru
Jina lake ni Mwamvua biti Masha.
Lakini kwa watu wa Dar es Salaam akivuma kwa jina la binti yake
Daisy kwa hiyo akijulikana kama Mama Daisy.
Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu Mama Daisy asingenieleza
chochote katika historia ya mumewe marehemu Abdulwahid Sykes.
Wakati ule watu walikuwa wakiogopa sana kusema lolote lililo kinyume
na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.
Jina la Abdul Sykes na mdogo wake Ally na wazalendo wengine kama
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint
Mzee, Iddi Faizi Mafongo, Oscar Kambona kuwataja wachache yote
yalikuwa yamefutwa kabisa.
Siku ile Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima
yaani Dar es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo
siku aliyosema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika
TAA yeye alipoingia TAA Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi
na akina Mama wa Dar es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.
Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa Mama Daisy.
Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe
walipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes.
Wanamajlis,
Mtakumbuka siku niliposema kuwa Mwalimu Nyerere alisema kuwa
hakumbuki cheo cha Abdul Sykes katika TAA palizuka ubishi mkubwa
sana hadi Yericko Nyerere kusema yeye ataiweka hapa hotuba hiyo
tusikize kama kweli Mwalimu Nyerere alitamka kweli maneno yale.
Mama Daisy hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa
ambalo lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae
ufalme, ''Baba yako yeye akimtaka sana Chief David Kidaha Makwaia
ndiyo aingie TAA wamchague president kisha waunde TANU.
![]() |
| Chief Daivid Kidaha Makwaia |
Lakini Chief hakutaka.
Kila Chief akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikuwa pale nikiwaandalia na
nikisika mazungumzo yao yote.
''Bwana Abdul akimwambia Chief Kidaha, ''David hebu achana na hao
Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''
Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu
kwa yale yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.
Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950.
Yako mengi lakini kwa leo haya yanatosha.
Anaetaka zaidi kuhusu Chief Kidaha Makwaia aingie hapa:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007
Pasco,
Naona nikuage na picha ya maalim wako Chama Omari Matata:
Kushoto: Ali Saleh, Mwandishi, Chama Omari Matata na aliyesimama nyuma ni
Balozi Mohamed Maharage BBC Club, Bush House London 1991

No comments:
Post a Comment