[QUOTE="MUSSA ALLAN, post: 15941747, member: 176958"]Dr.Dau alipoanza ku-qoute maneno kutoka kwenye msahafu nilitambua lengo lake papo hapo!
Kiongozi wa UMMA ukishajikita kwenye udini, jamii inakutapika! Mbaya zaidi watetezi wake hapa JF ndio wale wale magwiji wa kupandikiza chuki za kidini. Kama wewe na mwezio [USER=34266]Ritz[/USER][/QUOTE]
Mussa Allan,
Ikiwa unataka kulijua tatizo la udini msome P van Bergen (1981)
huyu ndiye mwandishi wa kwanza kulieleza tatizo hili.
Kisha msome John Sivalon (1992).
Halafu hitimisha na Hamza Njozi (2002).
Ukifanya haya tatizo la udini litakuwa halikupi shida hata kidogo.
Ukipenda sasa kupata picha kubwa na kujua nchi yetu ilikotoka
hadi tukafika hapa tulipo wewe ukisikia Qur'an unaogopa msome
mtu mmoja anaitwa Mohamed Said (1998).
Huyu atakuonyesha kwa ushahidi kuwa katika mikutano ya TANU
Sheikh Suleiman Takadir alikuwa anaanza kwa kusoma Surat
Fatha kisha ikaombwa dua na baada ya hapo ndipo anamkaribisha
Nyerere kuhutubia.
Nyerere ni Mkatoliki wala hakupata kuonyesha kukerwa na hilo.
Sasa hii jamii kutapika kwa kusikia aya za Qur'an kaleta nani?
Ukiwasoma hao waandishi niliokutajia hapo juu utajifunza mengi.
Hii mambo ya kukasirishwa na Qur'an ni mambo yalikuja baadae.
Dr. Dau alisoma aya hii:
''Fastabikul khyraat
Wafii dhaalika
Falyatanaafas
Almutanaafisuun.''
''Washindane katika kufanya mema wale wenye kushindana.''
Dr. Dau alisoma aya hii:
''Fastabikul khyraat
Wafii dhaalika
Falyatanaafas
Almutanaafisuun.''
''Washindane katika kufanya mema wale wenye kushindana.''
No comments:
Post a Comment