Tuesday, 19 April 2016

TOLEO JIPYA: ''CONFLICTS AND HARMONY IN ZANZIBAR'' NA ALI MUHSIN BARWANI


[​IMG]


Kitabu hicho hapo juu ni kumbukumbu za Ali Muhsin Barwani mmoja wa wapigania uhuru wa Zanzibar na kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) Hizbu. 

Akiwa mmoja wa mawaziri wa serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa mwaka wa 1964 Ali Muhsin alifungwa katika jela mbalimbali Tanzania Bara kwa miaka 10. 

Katika kitabu hiki Ali Muhsin anaeleza siasa za Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi na miaka aliyokuwa ''mfungwa wa Nyerere,'' kama alivyopenda kueleza mwenyewe. 

Baada ya kushindwa kupata pasi ya kusafiria baada ya kutoka kifungoni, Ali Muhsin aliamua kutoroka nchi kupitia njia za panya hadi Mombasa kisha Nairobi ambako alipokelewa na Umoja wa Mataifa na kutoka hapo akapata msaada wa kumfikisha uhamishoni Cairo.

Kitabu hiki ukikianza huwezi kukiweka chini.

Atakae kujua historia ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi kitabu hiki ni muhimu sana kwake.

Kinapatikana Ibn Hazim Media Centre, Msikiti wa Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House (TPH), Samora Avenue.

Bei ya kitabu ni Shs. 10,000.00


[​IMG]
Kulia: Ali Muhsin Barwani Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje,
Mohamed Shamte Waziri Mkuu na U Thant Katibu Mkuu UNO
Zanzibar ilipopata kiti chake UNO, 1963

No comments: