Sunday, 17 April 2016

KUTOKA JF: KAULI YA HAMZA MWAPACHU KWA UONGOZI WA TAA 1953



Matola,
Nitakujibu.

Waislam walikuwa wanapambana kwanza kama wazalendo na ndiyo
wakaasisi African Association 1929.

Kisha 1933 walewale walioasisi African Association wakaasisi tena
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika wakawa wanapambana kama
Waislam na sababu zipo.

Hapa ikawa ukoloni unapigwa pande mbili.

Ndiyo sababu Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walikwenda Nansio
1953 kupata kauli ya Hamza Mwapachu kuhusu kumtia Nyerere katika
TAA ili waasisi TANU mwaka unaofuatia na Nyerere wamchague rais wa
chama kipya.

Abdul Sykes alikuwa rais wa TAA na Ali Mwinyi Tambwe katibu wa Al
Jamiatul Islamiyya.

Ndiyo maana unaona viongozi wa kwanza TANU ilipoanzishwa 1954 wengi
walitoka Al Jamiatul Islamiyya na wnachama wa mwanzo wa TANU walitoka
Rufiji na waliandikishwa na Mzee Said Chamwenyewe.

No comments: