Umetia wasiwasi ambao hauna sababu.
Kwanza si mimi niliyeliita daraja hilo Daraja la Dau.
Jina hilo nimelipata Kariakoo.
Kila yanapokuja mazungumzo ya Dau basi likitajwa daraja
wataliita Daraja la Dau.
Mfano wa Rais Magufuli na Dau hauendani katika hili.
Rais Magufuli ni mkubwa wa nchi nzima.
Dr. Dau yeye alikuwa mkurugenzi tu wa taasisi iliyojenga
daraja.
Sasa kwa watu wa Dar es Salaam na khasa ukimchukulia
Dr. Dau alivyokuwa na mkabala na hawa nduguze kila lake
wao huliona lao.
Hii ndiyo sababu nadhani wakaliita daraja lile Daraja la Dau.
Hata mie siku nilipomwambia kuwa daraja linaitwa Dau yeye
alicheka.
Na unajua Dau kakulia Kariakoo utoto akicheza mpira Yanga
Kids na akina Tostao, Adolf Rishad na Kassim Manara na
hii imeongeza sana umaarufu wake hapa mjini.
Na umaarufu una bei yake.
Moja ni kama hili tunaloliongea hapa.
Najua fika kuna watu watakasirika wakisikia daraja linanasibishwa
na Dr. Dau.
Lakini tuna la kufanya kuzuia mapenzi ya watu?
Wanangu wananiuliza, ''Baba lini tutakwenda kuliona daraja la Uncle
Dau?''
Lakini haya ni ya kupita.
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika kuna sheikh mkubwa sana
katika TANU akihutubia wanachama wa TANU katika taarab Mtaa wa
Mvita kwenye tawi lililokuwa na nguvu kushinda matawi yote Tanganyika
alimwita Mwalimu Nyerere, ''Mtume wa Afrika.''
Wana TANU wenyewe waliona sheikh sasa kavuka mpaka na hili lilileta
farka kubwa sana ndani na nje ya uongozi wa TANU.
Mapenzi yakizidi yana khatari zake.
Dr. Dau ni mhanga wa watu wa Dar es Salaam kumpenda sana.
No comments:
Post a Comment