Monday, 4 April 2016

SULTANI GANI ANA SHUTUMA YA MAUAJI ZANZIBAR?

Utangulizi

SULTAN SAYYID ABDALLAH BIN KHALIFA BIN HARUB NA WANAE


Masultani 11 waliotawala Zanzibar 1856 - 1964

Hawa masultani 11 waliotawala Zanzibar kuanzia mwaka wa 1856 hadi 1964 kesho kiama siku ya hesabu watamkabili Mola wao mikono yao ikiwa haina damu ya mauaji wala utesaji wa ndugu zao Wazanzibari. Marehemu Aman Thani ameacha kumbukumbu muhimu ya hazina ya wakati mgumu katika historia ya Zanzibar. Aman Thani ameandika na kutoa mihadhara kadhaa akieleza hali ya wasiwasi na unyama iliyogubika Zanzibar baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1964.

Aman Thani
Itachukua muda kwa kizazi cha leo kuijua historia hii ya kusikitisha. Tuna wajibu wa kuisomesha historia hii si kwa nia ya kufukua makaburi na kutonesha makaovu bali kwa nia ya kuonyesha ubaya wa ubaguzi. Viongozi wa leo wana dhima kubwa kuhakikisha kuwa yale yaliyotokea Zanzibar nusu karne iliyopita hayajirudii tena.

No comments: