Saturday, 18 June 2016

KUTOKA JF: EARLE SEATON (BERMUDA) NA DOME BUDOHI (KENYA) KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA




Nguruvi3,
Mimi nakuhurumia sana tena sana kuwa hujui uwezo wako na hii
si hali nzuri.

Nimekuuliza na hukunijibu kwa kuwa uneingiwa na hofu ya jibu
langu.

Nakuuliza tena.

Je ungependa kujua jibu la jopo la waandishi wa historia ile ya
Chuo Cha Kivukoni walipopewa ''notes'' za Abdul Sykes kuhusu
historia ya TANU?

Daisy katika kuandika historia ya babu yake kaandika habari 
kutoka 1894 - 1949 tena akitumia mswada wa alioandika Kleist.

Nyerere ataingia vipi katika historia hiyo iliyoandikwa na Kleist 
kabla ya kifo chake 1949?

Ndipo ninapokuhurumia kuwa hujui ukomo wa uwezo wako na 
sasa unakuwa kichekesho.

Hiyo ''idea,'' mpya unayozungumza ya 1950 haikuletwa na Nyerere
kwa kuwa 1950 hakuna aliyekuwa anamfahamu katika siasa za TAA
pale New Street.

Hiyo ''broad coalition'' unayoizungumza ilianza 1950 kupitia TAA 
Political Subcommittee baada ya Abdul na Kyaruzi kuingia katika 
uongozi.

Hakuwa Nyerere aliyeibadili TAA kuwa TANU.

Mchakato huu ulianza 1950 na katika watu waliokuwa na msaada 
mkubwa katika hili ni Earle Seaton kuisaidia TAA kuandika katiba 
ambayo Gavana Twining aliikataa.

Nakuwekea picha ya Earle Seaton akiwa na Nyerere baada ya 
uhuru.

[​IMG]

Nyerere alipokuja kuingia madarakani 1953 alikuta kazi kubwa 
ilikuwa tayari ishafanyika.

Nakuwekea hapa uongozi wa TAA pale New Street mwaka wa 1953:
President, Julius Nyerere, Vice-President Abdulwahid Sykes
General Secretary Dome Okochi, Assistant Secretary Dossa Aziz
Treasurer John Rupia, Assistant Treasurer Ally Sykes.
Nakuwekea picha ya Dome Okochi Budohi hapo chini:

[​IMG]

Nguruvi3,
Hayo mengine uliyoandika ni vichekesho vikubwa sitakujibu chochote
ila hili la Sheikh Hassan bin Amir.

Ikiwa unataka kujua sababu ya mapambano ya Sheikh Hassan bin Amir
na Nyerere yaliyodumu kati ya 1963 - 1968 fungua uzi In Shaallah nitatoa 
darsa na ninalihakikishia barza hatomtumwa mtoto dukani.

No comments: