Saturday 18 June 2016

KUTOKA JF: BARUA YA AFRICAN ASSOCIATION 1933 ILIYOANZA KWA ''BISMILLAH RAHMAN RAHIM''








[​IMG]

Kushoto aliyesimama ni Ally Kleist Sykes, na kulia kwake ni
Abdulwahid Kleist Sykes, mbele kushoto ni Kleist Sykes 
Mbuwane na Abbas Kleist Sykes. Katika hawa aliye hai ni Abbas
Ukoo huu umeacha kumbukumbu nyingi kwa maandishi katika harakati za
kuunda African Association 1929 na kuunda TANU 1954. Picha hii imepigwa
mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam kutoka Lower Kabete Kenya
alipokuwa akipata mafunzo ya kijeshi katika King's African Rifles kabla
hajakwenda Burma kujiunga na Burma Infantry. Angalia utaona Abdul amevaa 
sare ya Jeshi la Mfalme wa Uingereza. Ilikuwa akiwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia
(1938 - 1945) ndipo alipoamua kuwa 6th Battalion iliyokuwa na askari kutoka 
Tanganyika waunde TANU wakirudi Tanganyika kudai uhuru.


Kashata,
Historia hii si ya akina Sykes peke yao.

Unajua katika historia ya uhuru na historia ya asili ya vyama vya siasa
Tanganyika huwezi ukaitafiti na kuandika kwa uhakika bila kuitaja AA.

Huwezi kuitaja African Association bila kumtaja Kleist Sykes.

Huwezi kumataja Kleist bila kuwataja watoto wake kwa kuwa wote
walishiriki katika uongozi wa African Association na kisha kuasisi TANU.

Lakini pia ukiwaleta hawa wanae itakubidi uwalete vijana wenzao wa
wakati wao waliokuwa katika siasa kama Hamza Mwapachu, Dr.
Kyaruzi,Tewa Said Tewa, Zuberi Mtemvu, Dr. Michael Lugazia,
Dossa Azizi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dustan
Omari, Dr. Luciano Tsere, Kasella Bantu 
kutaja majina machache.

Lakini tena na hili lina nafasi ya peke yake hutoweza kuwafikia wazee
kama Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi, Mshume Kiyate,
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Tatu
biti Mzee, Bi. Titi Mohamed 
na wengineo bila kupita kwa Abdul Sykes.

Haya yote ni kwa kuwa kwa wakati ule Tanganyika inaamka katika siasa
za utaifa hawa ndiyo walikuwa katika uongozi wa TAA na walikuwa watu
maarufu katika mji wa Dar es Salaam.

Dar es Salaam ya wakati ule Uislam ulikuwa na nguvu sana mgeni yoyote
asingeweza kufanya lolote bila ya kuungwa mkono na watu hawa.

Ukweli ni kuwa bila Abdul, Nyerere asingepokelewa.
Nitakupa mifano miwili.


Erika Fiah
Mwaka wa 1933 Kleist aligombana na Erika Fiah katika uongozi wa AA
na Kleist akajiuzulu uongozi na Fiah akachukua nafasi ya Kleist ya katibu.

Rais alikuwa Mzee bin Sudi.

African Association haikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na Mzee bin Sudi
ilibidi amwandikia Kleist barua kumsihi arudi katika uongozi.

Barua hii ya mwaka wa 1933 mimi nimeisoma na Mzee bin Sudi ameandika
kwa kuanza na ''Bismillah Rahman Rahim.''

Kleist alirudi katika uongozi.

Mwaka wa 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA kutoka kwa Abdul
Sykes 
chama kilikufa ikabidi juhudi zifanyike kukiweka chama katika hali
madhubuti hadi kufikia kuunda TANU.

Kwa kuhitimisha.

Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU haya waliyajua na ndiyo
maana kitabu kizima Abdul Sykes alikwepwa kutajwa na historia ikaanza na
Nyerere kwani walitambua wakimtaja Abdul na kueleza historia yake itabidi
wamtaje na baba yake na wengine wote kama nilivyoeleza.

Hili hawakulitaka.


Mwandishi akimhoji Abbas Sykes katika kipindi cha televisheni TV Imaan

No comments: