Kuna hii Picha imesambazwa katika mitandao ya ki jamii ikimkashif huyu mwanamke ati anakunywa maji mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Suala: Nani anajuwa Picha hii imepigwa wapi, saa ngapi, na katika mazingira gani?
Suala: Nani anajuwa Picha hii imepigwa wapi, saa ngapi, na katika mazingira gani?
Suali: Nani anamjuwa alikuwa katika hali gani wakati anakunywa Maji haya?
Sisi wanawake wa Ki Islam tunapokuwa katika siku za hedhi au nifasi (damu ya uzazi) basi hatupaswi kufunga, kusali, wala kushika kitabu kitakatifu cha Quraan mpaka damu ikatike na kujitahirisha tuwe Tahir. Tukisha maliza hedhi au nifasi baada ya Ramadhan tunalazimika kulipia swaum ila sala ndo hatulipi.
Katika siku hizo ambazo hupaswi kufunga basi pia ni dhambi kukaa na njaa bila kula au kunywa maana unatakiwa usifunge. Sharia zinamkataza mtu yoyote kula hadharani hata akiwa "Maadhura" au mgonjwa au yuko kwenye safari ya shida. Anatakiwa ale faraghani kama alivyofanya mwanamke huyu. Aibu ni ya huyo alompiga picha na kumkashif.
Si uzuri kumhukumu mtu wa dini usioijuwa sharia zake. Kusema anakazia saumu au anajiwahi na kadhalika ni kejeli kwa kitu usichokijua.
Katika Uislam kula au kunywa faragha ni sunna na ni aibu kama tunavyoona baadhi ya watu wakiwemo wanawake wanabugia mi burger mi chips barabarani kama majendaheka. Wanawake wa ki Islam tunatakiwa tujistiri saa zote ki mavazi na kimatendo ingawa wengi hatufati. (Allah atuhidi) Amin.
Waislamu hatwendi miskitini na vi mini na backless dresses kama baadhi ya waumini wa dini nyengine wafanyavyo ambapo sehemu za dini zinageuzwa hunting grounds for zinaa.
Tukianza malumbano ya dini kwa kukejeliana basi hiyo ni game that two can play at.
Kudos to this woman who has been ridiculed and humiliated by doing what her religion wants her to do!


No comments:
Post a Comment