Mbetini,
Kwanza nakushukuru kwa kuileta picha hii hadharani.
Mimi ndiye mtu wa kwanza kuiona picha hii nje ya wenyewe.
Hii picha nilipewa na watoto wa Sheikh Abdallah Chaurembo
katika miaka ya 1980 na mimi nilifanya mipango ipatikane nakala
yenye ubora na hilo lilifanyika.
Picha hii ilipigwa 1956 shambani kwa Sheikh Abdallah Chaurembo
Mtoni Dar es Salaam.
Ukoo wa Chaurembo una kawaida ya kufanya hawli kila mwaka na hii
inaendelea hadi leo
Katika hawali ya mwaka ule Mwalimu Nyerere alialikwa.
Pamoja na Nyerere kuna watu wengi maarufu katika picha hiyo.
Nyerere amekaa katikati ya Liwali Ahmed Saleh kushoto na SheikhBilal Mshoro kulia.
Yupo Rajab Diwani, Liwali Ahmed Saleh, Sheikh RamadhaniAbbas, John Rupia, Sheikh Bilal Mshoro kutoka Tabora, Saleh
Uchaguzi wa Kura Tatu, katika watoto waliokaa chini yuko Said
Mahfoudh mmoja wa vijana wa kwanza kuingia Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam katika miaka ya awali ya 1960.
Hii picha ilipotea kwa miaka zaid ya 20 hata wenyewe akina Chaurembo
wakawa hawana nakala ya picha hii.
Nimefurahi kuiona tena hii picha.
Alhamdulilah.
No comments:
Post a Comment