Friday, 24 June 2016

KUTOKA JF: KENNETH DAVID KAUNDA KATIKA HISTORIA YA TANU 1953







Bakar..,
A fascinating and amazing story in deed!

Kisa cha kukataliwa historia ya Abdul Sykes ni kuwa ikiwa utamleta Abdul
katika historia ya TANU itabidi urudi nyuma miaka miaka 50 kupata asili yao
ya Kizulu vipi walikuja Tanganyika.

Utakwenda hadi Kwa Likunyi Mozambique ambako Sykes Mbuwane babu
yake Abdul alikotokea.

Hiki kijiji kipo Imhambane na ndipo Von Wissman alipokwenda kuchukua
jeshi la mamluki wa Kizulu kuja Tanganyika kupigana na Abushiri bin
Salim
 na Chief Mkwawa miaka ya mwisho ya 1800.

Ally Sykes mwaka wa 1952 alichukua likizo na akaenda hadi kwao kwa
Likunyi kuona alikotoka babu yake.

Nimeandika kitabu cha maisha ya Ally Sykes, ''Under the Shadow of British
Colonialism.''

Huu mswada haujachapwa sasa karibu mwaka wa ishirini.

Humo ndimo aliponieleza safari tatu muhimu kwake wakati wa kudai uhuru.

Safari ya kwanza hii ya Mozambique 1952, safari ya pili Ghana kuadhimisha
uhuru wa Ghana 1957 tena hakupanda ndege kenda kwa nchi kavu na safari
nyingine ya Rhodesia 1953 alipokamatwa na Makaburu.

Safari hii TAA ilialikwa Northern Rhodesia na Kenneth Kaunda rais wa African
National Congress na alifatana na Denis Phombeah.

Ukielezwa aliyoshuhudia Ally Sykes katika hizi safari utajua nini maana ya ukoloni.

Ikiwa utaeleza haya na mengine mengi ambayo hapa hakuna nafasi ya kuyaeleza
utakuja na sura nyingine kabisa katika historia ya TAA, TANU na harakati za uhuru.

Itabidi ueleze vipi hawa akina Sykes walijuana na Kenneth Kaunda, Jomo
Kenyatta
,viongozi wa Fabian Society kama John Hatch kabla hata 
Nyerere hajawajua.

Itakubidi pia ueleze vipi baba yao aliasisi African Association (AA) 1929 na
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Vipi aliweza kujenga nyumba hiyo ilipozaliwa TANU na kujenga shule jengo
ambao lipo hadi leo.

Itabidi pia ueleze viongozi wa wakati ule na michango yao katika jamii hasa
machifu kama Chief Kidaha Makwaia, Chief Abdallah Said Fundikira na
Thomas Marealle ambao wakijuana vyema na akina Sykes na kustahiana
sana.

Hizi ndizo zilikuwa siasa za nyakati ule.
Haya hayakutakiwa.

Waandishi na watafiti wa Kivukoni College waliona hii itapunguza umuhimu wa
Nyerere katika historia ya TANU.

Tatizo likawa historia ya TANU lazima ianze na Mwalimu Nyerere.
Hili ndilo likasababisha matatizo mengi katika uandishi wa historia ya TANU.

Hivi ndivyo tulivyofikishwa hapa leo tuko barzani tunajadili na wengine kama
akina Nguruvi3 wanajadili kwa hamaki wakidai ati Mwalimu Nyerere
anakashfiwa.

Na ''kashfa,'' yenyewe ni kule kuandika historia ya TANU kama ilivyokuwa.







Onyx,
Huna haja ya kuchanganyikiwa wala kumtafuta 
Kaunda.

Mimi sikwenda Zambia kuyajua haya yote.

Unachotakiwa kufanya ni kupitia Sykes Papers.

Hebu soma hapo chini:
''In his capacity as the secretary of TAGSA, Ally
Sykes 
had established contact with the Secretary
-General of the Pan African Congress of Northern
Rhodesia, Kenneth David Kaunda.'' [1]


[1] K.D. Kaunda to A.K. Sykes, 28 th December,
1953. Sykes Papers.

Kutoka kitabu cha Abdul Sykes...

No comments: