Othman na Nyerere, Prof. Haroub alipomwambia Nyerere, ''MwalimuWembee,
Mchango wa Nyerere katika TANU na kudai uhuru ni mkubwa sana.
Ikiwa nitajaribu kusema kuwa Nyerere hakuwa lolote katika historia ya
Tanganyika nitakuwa nimejivunjia heshima yangu.
Ukisoma kitabu changu utakuta sehemu nyingi ambazo zinaeleza vipi
Nyerere alijenga matumaini ya Watanganyika katika kurejesha utu na
heshima yao.
Ila hutomsoma peke yake.
Ikiwa ni katika mikutano ya mwanzo 1955 pale Mnazi Mmoja utamsoma
Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, Bi. Titi Mohamed na wengineo.
Ikiwa safari ya kwenda UNO utamsoma Nyerere na Idd Faizi Mafongo,
Mwalimu Kihere na wengineo.
Ikiwa sakata la kura tatu utamsoma Nyerere na Sheikh Rashid Sembe
na Hamisi Heri na wengineo.
Hutomsoma Nyerere peke yake.
Utakapokuja katika kuasisi TANU utasoma nimeandika historia ya TANU ni
historia ya maisha ya Abdul Sykes na katika maisha hayo pia utamkuta
Julius Nyerere, Hamza Mwapachu na wengineo.
Hapa ndipo ilipo tofauti baina yako na mimi.
Ikiwa wewe utaona huu ni udini hii ni bahati mbaya kwa upande wako.
Nasema ni bahati mbaya kwa sababu kitabu changu kimefanyiwa ''review,''na
mabingwa wa historia ya Afrika duniani kama John Iliffe, James Brenan,
Jonathon Glassman na wengineo.
Hili la udini hakuna hata mmoja ameliona isizidi ndiyo ikawa sababu ya mimi
kualikwa kwenye vyuo vyao kuzungumza.
Hakuna alomfuta Nyerere katika historia ya TANU lakini wapo waliomfuta
Abdul Sykes katika historia ya TANU na Nyerere alikaa kimya.
Ikiwa unadhani historia ya TANU na historia ya Nyerere imeandikwa basi nakuhakikishia
historia hiyo ndiyo sasa inaandikwa.
Chanzo cha kuiandika historia hii ni mazungumzo kati ya Prof. Haroub
lazima uwajibu Ali Muhsin na Mohamed Said.''
Said:
Majibu ni kwa ajili ya vitabu walivyoandika na Ali Muhsin na Mohamed
Wembee,
Soma vitabu hivi utakudhihirikia kweli kuwa historia ya Tanganyika
ilikuwa bado haijaandikwa.
Hao maprofesa unaowaona hapo chini ndiyo sasa wanaandika historia
ya Mwalimu Nyerere ambayo ndiyo historia ya TANU na historia ya uhuru
wa Tanganyika:
Prof. Saida Othman na Prof. Issa Shivji aliyekaa chini ni Mwandishi katika mahojiano
kuhusu Mwalimu Nyerere na TANU nyumbani kwa mwandishi.
No comments:
Post a Comment