Monday, 27 June 2016

KUTOKA JF: PROF. ALI MAZRUI NA PROF. MOHAMED BAKARI









Mtebetini,
Mwaka wa 2003 katika mkutano wa Kimataifa Kampala, Uganda ambao kati ya
waliowasilisha mada alikuwa Prof. Ali Mazrui na Prof. Mohamed Bakari,
Prof. Mohamed Bakari katika kufanya majumuisho ya yale aliyosikia pale
alisema kuwa ni muhimu Waafrika wakaandika historia yao wenyewe kwani
wakiacha historia yao iandikwe na watu wengine wataandika mambo ambayo
wao hawatayapenda.

Prof. Mazrui halikadhalika Prof. Mohamed Bakari wameandika mengi ambayo
yamesaidia sana katika kufahamika mengi katika Afrika.

Lakini hawa walikuwa wasomi waliobobea katika fani zao.

Sasa ukitazama hayo yaliyoandikwa katika uzi ulionielekeza niusome kwa kweli
kuna makosa mengi si tu ya ukweli wa hayo yaliyoandikwa bali hata makosa ya
lugha na kukosekana kwa rejea za kuthibitisha kuwa mwandishi alifanya utafiti.

[​IMG]
Prof. Mohamed Bakari akiwa ofisini kwake Fatih University Istanbul, Turkey na Mwandishi

[​IMG]
Kulia kwa Prof. Mazrui ni Tamim Faraj Muslim University
of Morogoro (MUM) na kushoto kwake ni Mwandishi
Hilton Hotel, Kampala 2003

Wanamajlis,
Ingieni hapo chini msome dunia inasema nini kuhusu Prof. Ali Mazrui ili muweze
kupima kama kweli kila mtu anaweza kushika kalamu akaandika kuhusu historia
ya Afrika:

http://www.mohammedsaid.com/2014/10/taazia-ya-prof-ali-mazrui-1933-2014.html

No comments: