Monday, 27 June 2016

KUTOKA JF: MWALIMU NYERERE NA MCHEZO WA BAO





Picha:Nyerere bao butiama.jpg

Wembeee,
Kwani ndugu yangu mtu ikiwa kazi yake ni kuuza samaki ndiyo
hairuhusiwi kuandika makubwa aliyochangia katika jamii?

Au mtu akiwa anacheza bao ndiyo yeye keshapoteza heshima
yake na hastahili kutajwa?

Mwalimu Nyerere alipokuwa mtoto mdogo siku moja chifu wa
jirani alimtembelea Chief Burito akamkuta Nyerere yuko nje
anacheza bao.

Yule chifu akamwambia Nyerere hebu cheza na mimi.
Hii ilikuwa katika njia ya mtu mzima kufanya maskhara na mtoto.

Yule chifu alipata mshtuko.
Mwalimu Nyerere alimfunga.

Alipokuwa faragha na Chief Burito Nyerere akamwambia huyu
mtoto hebu mpeleke shule akasome kwani ana akili sana kanifunga
bao hapo nje.

Hizi habari ziko katika kitabu cha Morlon (2015).
Kinapatikana Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.

Kama wapendavyo kusema Waingereza, ''The rest is history.''
Nyerere alikuwa mcheza bao maisha yake yote.

Babu yangu aikuwa mcheza bao maisha yake yote na wazee wangu
wengine wengi tu walikuwa wacheza bao.

Mwanzoni nilidhani wewe ni muungwana na kijana ulieleka sawa kumbe
nilikosea.

Prof. Juma Kapuya alikwenda Butiama akamkuta Mwalimu Nyerere
kwenye bao.

Mwalimu akanyanyua kichwa chake akamwambia Kapuya, ''Kaa hapo
nikufunge kama mtoto mdogo.''

Kapuya hakuthubutu.

Dar es Salaam Mtaa wa Mafia na Kongo karibu na nyumba ya Mzee Maneno
Kilongora
 kulikuwa na barza kubwa ya bao.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Tabora 
alikuwa akenda pale kushindana na mabingwa wenzake.

Bao ni moja ya mila zetu.
Kama ilivyo kwenu kwenda kilabuni kunywa pombe za kienyeji.

Msome babu yangu ''Mcheza Bao,'' hapo chini uone nini alifanya katika
historia ya Tanganyika:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH

No comments: