Pasco,
Hakuna anaekataa kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeoongoza mapambano dhidi
ya Waingereza.
Historia hii imeandikwa na sote tunaikubali ila ninachosema mimi ni kuwa mbona
hakuwa peke yake katika mapambano hayo?
Licha ya hilo kuwa hakuwa peke yake ninachosema mimi ni kuwa mapambano ya
kudai uhuru yalianza kabla yake.
Na kuthibitisha hilo ndipo nikaandika kitabu cha Abdul Sykes nikitumia njia ya
''biographical approach.''
Nimekuwekea Kamati ya Siasa katika TAA ambayo Abdul Sykes aliipa jina la TAA
Political Subcommittee kama nyaraka zake zinavyoonyesha na hii ilikuwa 1950.
(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951.
Sykes' Papers).
Katika taarifa hii Abdul kaeleza mengi kuhusu juhudi za kuja na chama cha siasa.
Soma kitabu changu yote nimeeleza kwa urefu na mapana yake.
Nyaraka hizi zipo na sasa zina umri wa miaka 66 na zilikuwa mikononi kwa marehemu
Ally Sykes hadi alipofariki.
Abdul Sykes awe muongo mkweli uwe wewe kwa kuzungumza na Omari Matata
ambae hakuna anaemjua katika histori ya Tanganyika?
Nyerere hakuweko katika kamati hii.
Nimekuwekea majina ya wanakamati wote na hawa ndiyo waliouanda TANU 1954.
Lipi la uongo nililosema mimi.
Sasa ngoja nije katika saikolojia ya watu unaodai kuwa ulizungumzanao kuhusu
historia ya TANU.
Labda hukuwa unajijua wala hukuwa unajua hali ya wakati ule ulipozungumzanao.
Kwa watu hawa kama Sheikh Kassim Juma na Nurdin Hussein wewe ulikuwa
mpelelezi umetumwa kuwachimba na ndiyo maana wakakufurahisha kwa kukupa lile
ambalo ndilo lililokuwa likitakiwa liwe.
Mimi Sheikh Kassim ni kaka yangu.
Aliwekwa ndani na hiki ni kisa mashuhuri.
Kuna khutba imepewa jina, ''Leo Nitataja Majina.''
Siku alipotoa khutba hii mimi nilikuwapo ilikuwa katika khutba ya Ijumaa Msikiti wa
Mtoro huu ndiyo wakati ule alipokuwa anapambana na serikali kuhusu madhila ya
bucha za nguruwe.
Hiyo ndiyo siku hadharani Waislam walimsikia Sheikh Kassim akieleza historia ya
Abdul Sykes na Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Jiulize kipi kilichomfanya Sheikh Kassim kuvunja mwiko siku ile?
Mwiko uliokuwa umehifadhiwa kwa zaidi ya miaka 40?
Siku ile pia alimtaja na Rajab Diwani.
Mimi nimeishi ndani ya historia hii na hao wote ninaokutajia wakinijua
na mimi nikiwajua ingawa nilikuwa kijana na mdogo kwao wote.
Nawafahamu vizuri kila mmoja wao na misimamo yao ya siasa.
Pasco,
Wewe ni mgeni kwa watu hawa.
Sheikh Nurdin Hussein ni mzee wangu.
Nawajua wanae tumekua sote Kariakoo.
Sheikh Nurdin Hussein alihidhuria mkutano ule wa Mtaa wa Pemba
wa 1955 ambao Sheikh Hassan bin Amir alitoa wazo kuwa TANU
ichukue kwa makusudi mwelekeo wa ''nationalist-secularist party.''
Nina hakika Sheikh Nurdin alikuficha haya hakukueleza kwa kuwa
hakuwa anakuamini wala kukufahamu umetokea wapi.
Sheikh Nurdin aliwekwa ndani na Nyerere na kupelekwa uhamishoni
Ngombezi labda hilo pia hakukueleza.
Sheikh Ali Comorian rika langu mchezo wetu mmoja.
Baba yake Sheikh Ali Mzee Comorian alifungwa na Nyerere wakati
Sheikh Hassan bin Amir alipokamatwa na kufukuzwa Tanganyika 1968.
Kwa wote hao niliokutajia mimi si ''outsider,'' kama wewe.
Hawa ukienda wewe kutaka kuwauliza historia ya TANU tayari ushawatisha.
Hao wengine katika masheikh uliowataja wala sioni kama ipo haja ya kusema
lolote.
Mwisho mimi sijapatapo kumbeza Nyerere siwezi kukosa adabu kiasi hicho
na kama una ushahidi wa hili ulete hapa barzani watu wote waushuhudie.
Ila mimi siwezi kumpa Nyerere sifa isiyokuwa yake wala siwezi kumdhulumu
kwa lile ambalo kwa hakika anastahili kusifiwa.
Historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika ni mimi niliyokuja kuikamilisha.
Pasco,
Nakuwekea kumbukumbu muhimu:
Sheikh Kassim siku alipotolewa jela hapa ni Msikiti wa Mtoro
Ingia hapa usome historia ya Sheikh Kassim bin Juma hii ni mada niliwasilisha Chuo Kikuu
Cha Kenyatta, Nairobi:
Mohamed Said: Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma (1940 – 1994) And the Dar es Salaam Pork Riots of 1993
No comments:
Post a Comment