Katka vitu vya kujivunia mtu wa Tanga katika Historia ya Tanganyika na Tanzania kwa ujumla basi ni pamoja na mtu huyu Hamza Kibwana Bakari Mwapachu, baba yake Harith Bakari Mwapachu(mbunge mstaafu Wa Tanga), Rahma Mark Bomani, Juma Mwapachu, Wendo Mtega Mwapachu, Tunu Mwapachu na Jabe Jabir Mwapachu. Hata Mohamed Said katika kitabu chake cha ' The Life and Times of Abdulwahid Sykes' ameandika pamoja na haya kuhusu Dr Hamza Mwapachu Rafiki Wa karibu Wa Marehemu Abdulwahid Sykes, Dosa Aziz na Mwalimu Nyerere:
"midst this power struggle and on the side of the up-and-coming young men was a Makerere graduate, a Digo from Tanga named Hamza Kibwana Mwapachu who we have already mentioned. Mwapachu was employed by Community Development Department as Assistant Welfare Officer in charge of Ilala Welfare Center in Dar es Salaam. Mwapachu's political career began at Makerere College where he was involved in student politics in the period between the two world wars. In 1946 while at Tabora, Mwapachu was elected African Association Secretary with Julius Nyerere as his deputy."
May Almighty God grant him Jannah-Paradise!
Mohamed Said Salum Sheikh kuna hiki kisa amenihadithia Juma Mwapachu.
Wakati
akiwa Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki alikutana na Ali Mwakwere.
Mwakwere
amepata kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Waziri wa Uchukuzi Kenya.
Binafsi nimepata kumuona Mwakwere Lamu kwenye Maulid maarufu ya Lamu ya kila
Mfungo Sita.
Sasa Juma Mwapachu alipokutana na Mwakwere haikuwa tabu wao
kujuana kuwa ni Wadigo kutokana na majina. Katika mazungumzo Mwakwere
akamwambia Juma kuwa yeye ni Mdigo wa Kwale na Juma hali kadhalika akamwambia
yeye kwao Gombero na ni mtoto wa Hamza Mwapachu.
Mwakwere alipojua kuwa Hamza
Mwapachu ndiye Mdigo wa kwanza kuingia Makerere College alipofika Kwale akaomba
Kwale Council imuadhimishe Hamza Mwapachu kwa kumpa mtaa na hili likafanyika.
Ukifika leo Kwale upo mtaa unaitwa Hamza Mwapachu Street. Hamza ana mtaa Kenya
ugenini hana mtaa kwao Tanga.
Haya ndiyo maajabu ya historia ya Tanzania.
Ingia ofisi ndogo ya CCM Lumumba hakuna hata picha ya pamoja ya wazee waliokuwa wajumbe wa Baraza la TANU.
Yusuf
Makamba anapewa Mtaa Gerezani Dar es Salaam karibu kabisa na mtaa aliokuwa
akiishi Dossa Aziz, Mtaa wa Mbaruku.
Huu mtaa wa Mbaruku ni mtaa ambao babu yangu alikuwa na nyumba katika miaka ya 1930 na aliiuza mwaka wa 1947 alipohamia Tabora.
Dossa hana kumbukumbu yoyote Dar es Salaam
juu ya yote yale aliyomfanyia Nyerere, TANU na Tanganyika.
Ukiwauliza hao waliompa Makamba mtaa katika Jiji la Dar es Salaam kafanya lipi kubwa sijui watajibu kitu gani?
Labda lile la Mwembechai mwaka wa
1998.
No comments:
Post a Comment