Sunday, 31 July 2016

KUTOKA FB: ''WAHAINI'' NA ''MAFISADI'' WALIOWEKWA KIZUIZINI BILA YA KUPELEKWA MAHAKAMANI

KATIBA TULIYONAYO IKITEKELEZWA KWA 100% RAIS WETU ATALAUMIWA KUWA DICTATOR. . KUMBUKENI KATIBA HII ALIITUMUA BABA WA TAIFA KUWAWEKA DETENTION WAHAINI NA MAFISADI WENGINE BILA KUPELEKWA MAHAKAMANI.

Mohamed Said Salum Musham Mzanda hawa waliwekwa kizuizini: Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi. 

Kushoto: Mwandishi, Sharif Hussein Badawy, Abdallah Miraj, Abdallah Tambaza
na Abdallah Kageta 

Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. 

Baadhi yao walikamatwa kwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani wa Nyerere. 


Bilal Rehani Waikela
Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusika na msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakati huo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendesha madrasa yake kila magharibi pale msikitini. 

Maalim Mohamed Mattar
Shariff Hussein na nduguye Mwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwa wamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababu walikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy. 

Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwa akifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. 

Sheikh Hassan bin Amir yeye hakuwekwa kizuizini ila alifukuzwa Tanganyika.


(Halikadhalika Sharif Hussein alifukuzwa pamoja na mdogo wake Mwinyibaba wakarudishwa kwao Kenya). 

Alionekana ni tatizo kwa kuwa alikuwa anataka kuwajengea Waislam Chuo Kikuu kupitia East African Muslim Welfare Society (EAMWS) chama hiki kikapigwa marufuku na Nyerere akawaundia Waislam BAKWATA. 

Bwana Muvanda nimeona nikueleze haya ili uwe na upande wa pili wa habari. 
Hawa hawakuwa wahaini wala mafisadi. 

Walikuwa Waislam wema na wengi wao walipigania uhuru wa Tanganyika. 

La unataka kujua mengi zaidi soma kitabu: ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika'', Minerva Press London 1998.

Unaweza kusoma historia za baadhi ya hawa niliowataja hapo chini:

No comments: