Monday, 1 August 2016

KUTOKA JF: MAREHEMU ABBAS KILIMA ALIVYOWANUSURU WAISLAM KATIKA MGOGORO WA SHULE YA KINONDONI


Kulia: Sheikh Abbas Kilima Sheikh Salum Khamis na mbele ni Sheikh Abubakar Mwilima
(Wote ni marehemu)








Gangongine,
Hii ishakuwa pembea la mzunguruko tulokuwa tukipanda Mnazi Mmoja
siku ya Eid.

Hebu sema kitu kuhusu Bergen (1981)Sivalon (1992) na Njozi (2002).
Sema kitu kuhusu hujuma za Chuo Kikuu Cha Waislam cha EAMWS 1968.

Sema kitu kuhusu Chuo Cha Kiislam cha OIC kilichotaliwa na serikali kujengwa
Tanzania.

Sema kitu kuhusu Shule ya Ufundi iliyotaka kujengwa na Darul Iman, Kibaha
ikapigwa vita na ''lobby.''

Sema kitu kuhusu marehemu Prof. Malima alivyopigwa vita na ''lobby,'' kisa
nini?

Nakuachia wewe utoe jibu kama kweli wewe unaijua historia ya nchi yetu.
Sema kitu kuhusu Shule ya Masjid Quba iliyokataliwa kupewa usajili na serikali.

Waislam hawaruhusiwi kujiendeleza na mawakala wa kanisa ndani ya serikali
ndiyo wanaongoza hujuma hizi.

Unakuja unanambia nieleze jitihada za kujiendeleza.

Hivi hujui mkasa wa shule ya Kinondoni na Kibohehe zilizojengwa na EAMWS
vijana wa Warsha walipozichukua na zikatoa 1st class kuwa zilivamiwa na viongozi
wake akina marehemu Mussa Mdidi na Burhani Mtengwa kuandamwa na
amri ikapitishwa kuwa hawana ruhusa kuongoza taasisi yoyote ya Kiislam?

Kosa lao nini kuzibadili shule za Kiislam kuwa kati ya shule bora nchini.

Huvu hujui kuwa na mwalimu wao Sheikh Hussein Malik akapigwa PI
na kufukuzwa nchini?

Hivi hujui kuwa na mapolisi wakatumwa kuvamia shule ya Kinondoni na
mkutano uliokuwa umepangwa wa Waislam kujadili hatua ya serikali
ukapigwa marufuku na aliyesoma tangazo hili kupitia Radio Tanzania
alikuwa David Wakati?

Dunia nzima ikasikia chombo cha umma kikitumika kuwapiga Waislam vita
ya kisaikolojia.

Askari aliyepewa kuongoza operesheni shule ya Kinondini alikuwa kijana wa
Kiislam Msafiri Himba kutoka Kituo Cha Oyster Bay.

Himba kwa hekima kubwa sana na uchungu wa dini yake aliwapenyezea
taarifa nduguze kuwa wasikaidi amri hapo kesho atakapowaambia waondoke
wafanye hivyo ili roho za waumini zinusurike.

Abbas Kilima aliyekuwa kiongozi wa Waislam alitumia busara na salama
ikapatikana.

[​IMG]
Wapili kushoto ni Sheikh Abbas Kilima (marehemu). Sheikh Kilima na hao unaowaona katika hiyo picha ndiyo walikuja kuasisi Baraza Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam Tanzania. Hii ni picha iliyopigwa ofisini kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu Augustino Mrema siku walipopewa tasjila baada ya kuhangaishwa sana na serikali.

Msafiri Himba hakupiga bomu la machozi wala risasi wala hakusumwa mtu
na hadi leo kila nikumkumbusha historia hii hunambia, ''Mimi namshukuru
Sheikh Abbas Kilima amri niliyopewa ilinifanya nisilale usiku kucha.''

Mbona tunajua mengi?
Wewe unadhani mimi niko hapa kufanya maskhara?

Huu ndiyo ukweli wa historia ya Waislam wa Tanzania.
Wewe kunuiliza mimi jitihada za Waislam ni sawa na kuuliza embe Kibada.

Lipi la Waislam ambalo Mohamed Said halijui?
Kwa historia zaidi ya mambo haya ingia hapo chini:
Mohamed Said: WARSHA
Mohamed Said: PROF. KIGHOMA ALI MALIMA: THE LAST DAYS...JULY/AUGUST 1995

No comments: