Thursday, 7 July 2016

KUTOKA JF: MALI ZA WAISLAM ZILIVYOCHUKULIWA NA KABIDHI WASII NA KUKABIDHIWA BAKWATA 1968


















G Sam,
Kuna kitu kimoja huwa kinatokea mara nyingi kunapokuwa na jambo la Waislam.

Mathalan umeandika unasema kuwa itakuwaje Wakristo na wengine na wao wakadai.
Historia ya Waislam na utawala wa Nyerere ni historia ya pekee.

Tatizo la Waislam hata siku moja haliwezi kufananishwa na shida ya jamii yoyote katika Tanganyika.

Kufanya hivyo ni kuudogosha Uislam na kuwadogosha Waislam.

Historia ya Waislam na mapambano yao dhidi ya ukoloni na kisha serikali huru ya Tanganyika ni kitu kingine kabisa kisicho na mfanowe.

Bahati mbaya historia ya Waislam si katika historia mbazo walio kwenye madaraka wangependa ienziwe na hii ndiyo sababu ya huu ujinga tulionao hivi sasa.

Hapa hapatoshi kueleza hayo lakini ukitaka kujua hebu soma hapo chini:

Msomaji,
Hapo chini ni mswada wa kitabu kama jina linavyoonyesha.

Kwa yeyote atakaesoma hata kama ni sura moja ataweza kujua siasa za
Tanzania zinavyoendeshwa. Ni kazi ambayo kwa uchache imechukua takriban
miaka ishirini na baadhi ya sura zimetoka katika mada ambazo zilipata 
kuwasilishwa katika mikutano na makongamano ndani na nje yaTanzania. 

Kazi hii kwa ukamilifu wake ilikamilishwa wakati mwandishi alipokuwa 
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin Ujerumani kama mtafiti mualikwa 
mwaka wa 2011. 

Wenyeji wake walimuomba kwa kipindi atakachokuwa hapo ZMO awaandikie na awaachie kazi mojawapo katika kazi zake. Mswada huu upo katika maktaba ya 
ZMO kwa mapitio kwa watafiti wanaofanya utafiti kuhusu historia na siasa Afrika 
na makhsusi wale wanaofanya utafiti kuhusu Tanzania.

Ingia hapo chini kusoma:
Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania

[​IMG]
Mwandishi akiwa ofisini kwake Zentrum Moderner Orient, Berlin 2011 akikamilisha uandishi
wa ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania.''


Huo hapa juu ulikuwa mukadama yaani utangulizi.

Nakuwekea hapo chini vipi mali ya Waislam ilichukukuliwa na serikali 1968
baada ya Nyerere kuivunja EAMWS:

''Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya
Kwikima, iliipa BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS.
Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali
alitoa taarifa fupi:

''Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi
la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la
East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini
ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.

Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa
nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu
Waislam peke yao.

Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili nakulitolea uamuzi
tatizo hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa
amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi
shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS
zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha
zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia
kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa
kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema
kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha
sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa
ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na
mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam
Nasibu. 


BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na
miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.

Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru
waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa.''
(Kutoka: ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...''

No comments: