Umenipeleka mbali sana.
Ilikuwa baada ya ''Takbira,'' kuashiria mwandamo wa mwezi kuingia
Mfungo Mosi na Eid kilichofatia katika radio ilikuwa mwimbo huu.
Ilikuwa baada ya ''Takbira,'' kuashiria mwandamo wa mwezi kuingia
Mfungo Mosi na Eid kilichofatia katika radio ilikuwa mwimbo huu.
Huyu ni Salum Abdallah na Cuban Marimba Cha Cha Cha Band.
Alikuwa rafiki ya baba yangu katika ujana wao 1950s.
Nakumbuka siku moja bibi yangu Zena biti Farijallah akiniambia
kuwa wakati baba yangiu yuko Tabora ilikuwa kila Salum Abdallah
akija mjini pale na band yake alishaweka vyombo vyake hotel basi
lazima aende nyumbani kwa baba yangu.
Wakati huu akirekodi na label inaitwa Mzuri ya Guy Johnson.
Huyu alikuwa Muingereza rafiki na Peter Colmore. Guy Johnson
alikuwa akienda mwenyewe kumrekodi Salum Abdallah
Morogoro.
Radio Tanzania wana hazina kubwa ya muziki wa Salum Abdallah
toka alipoanza kurekodi 1955.
Ziko nyimbo zake zimeharibika haziwezi kupigwa kama, "Moyo
Koma," "Nipo Chini ya Mkungu."
Sina hakika na kama hizi ni "title," zake khasa.
Lakini binafsi nazijua na tukiziimba katika utoto. 1964 nikiwa
na miaka 12 nilikutana na Salum Abdallah Mtaa wa Aggrey ilipokuwa
Cuban Branch alikuwa na wenzake wakifanya mazoezi.
Nilisimama nje nikamsikiliza kwa muda mrefu akipiga guitar
na kuimba hapa na pale akielekeza muziki.
Baada ya mwaka Salum Abdallah akafa kwa ajali na siku ile alikuwa apige
Community Centre Morogoro.
No comments:
Post a Comment