Saturday, 2 July 2016

KUTOKA JF: NI KWELI WAISLAM WAMEKATALIWA KUTUMIA UWANJA WA UHURU KWENYE SHEREHE ZA EID?


Wanamajlis,
Nimepokea taarifa hii leo asubuhi najaribu kupata ukweli:

[11:11am, 02/07/2016 WAISLAM WAKATALIWA KUTUMIA UWANJA WA UHURU KWENYE SHEREHE ZA EID.

*MWANZO WALIKUBALIWA NA WAKAAMBIWA WALIPIE Tsh 10,000,000/=

*BAADA YA KUTEKELEZA MAELEKEZO HAYO , IKAJA AMRI NYINGINE YA KUNYIMWA KIBALI CHA MATUMIZI YA UWANJA HUO.

*WAISLAM WATILIA SHAKA KUWA KUNA AGENDA YA SIRI, KWANI HAKUKUWA NA SABABU ZA MSINGI.

*WAISLAM WAOMBA RAIS KUINGILIA KATI.

* YATANGAAZWA KUPATIKANA KWA HASARA YA ZAIDI TSH. 50,000,000/= KWAJILI MAANDALIZI YA SHEREHE HIZO.


[​IMG]
Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Uwanja wa Uhuru yaliyotayarishwa na
Sheikh Nurdin Kishki Mwezi wa Ramadhani 2016
Mashindano yakuhifadhi Qur'an yalijaza watu kushinda mpira katika uwanja ule...ujumbe ule ni mzito kwani dunia nzima picha za Waislam walioshonana kusikiza Qur'an zilionekana...wengi bila shaka walisema, "Ala Tanzania kumbe Waislam wengi vile!" Hii inawezekana imewatisha wenye mamlaka ya kutoa na kutotoa, wenye mamlaka ya kuwasha na kuzima...

Ukiitazama hiyo picha unaweza kudhania Simba na Yanga wako uwanjani wanawania kombe la ubingwa lakini siyo umma umekuja kusikiliza Qur'an siyo kuangalia mpira.

Hii haijapatapo kutokea nchini petu.
Alhamdulilah...


Photo


Photo

Photo


No comments: