HISTORIA YA
KANISA LA MKUNAZINI
(ANGLICAN
CHURCH)
Zahir Al
Kharusi
Kwanza kabisa
ikumbukwe vizuri kuwa biashara ya watumwa kutokea Congo na Malawi ilisimamishwa
rasmi mwaka 1885 ndio ilikua mwisho utumwa Zanzibar na hapo Mkunazini karibu ya
Soko Kuu palikua na sehemu ya uwanja au kikataa kitupu na kibanda kidogo cha
makuti ndio mtu mwenye mtumwa wake nyumbani kwake humleta pale akanadiwa
akauzwa na wale watumwa wanaotokea Congo ma Malawi pia. Eneo hilo tupu halikuwa
na nyumba kubwa ya kudumu na ardhi hiyo ilikuwa ya Mhindi ambaye yeye aliitoa
ijengwe hospitali ya Doctor Mortan Waswahili wakaiita hospitali ya kwa
kimoto. Ujenzi wa kanisa hilo, hospitali, nyumba ya padri na wachungaji zote
zilianza kujengwa mwaka 1905, ni miaka ishirini iliyopita tokea kusimamishwa
utumwa hapa Zanzibar wakati wa Sayyid Barghash bin Sayyid Said Albusaidy mfalme
wa tatu wa kwanza ni Sayyid Said bin Sultan Albusaidy wa pili ni Sayyid Majid
bin Sayyid Said Albusaidy.
Kwa hivyo eneo
hilo halikuwa na jengo la kanisa nyumba za mapadri wala hospitali majengo yote
hayo yameasisiwa baada ya miaka ishirini kupita. Maneno na historia inayotolewa
kuwa palikuwa na soko ama nyumba iliokuwa ikifungiwa watumwa ni hadithi ya
uongo na uzushi lengo lake ni kupandikiza chuki kubwa juu ya Uislamu na Waarabu
wakati huyo David Livingstone huko kwao Uingereza na Marekani ndio
walinunua watumwa zaidi ya milioni kumi kutokea nchi za Afrika. Hapo Mkunazini
ulikua uwanja mtupu uliopakana na sehemu ya mnada wa vitu vya kawaida yaani
sokoni na ikawa ni urahisi mtu anayetaka kuuza mtumwa wake ampeleke eneo hilo
lilopakana na sokoni amuuze. Hakika nyumba iliokuwa chini ina eneo la chini la
baraza na mfano wa vyumba vya chini lilikuwa linatumika kuwekea madawa
yaliyohitajia ubaridi na usalama zaidi wa maradhi ya ndui (smallpox diseases)
yaliowahi kuwepo miaka ya 1910-1920 hapa Unguja.
Hakika uzushi
wa chuki uliowekwa hapo katika Kanisa la Anglican ni uzushi mbaya sana na wa
hatari na uliokuja kutiwa nguvu na Bibi wa Kizungu kutokea ‘’Nordic countries’’
alipoyachonga na kuyatengeneza masanamu kwa gharama kubwa sana huenda kapewa na
wanaouchukia Uislamu na Uarabu huko Ulaya kwa sababu ni masanamu makubwa na
kuyasafirisha kutokea Ulaya mpaka hapa Zanzibar ilikuwa ni gharama kubwa na
bila ya kuchukua tahadhari Idara ya Nyaraka za Kale na Idara ya Mila na Utamaduni
Zanzibar waliyaruhusu masanamu hayo kuingia nchini na waliyaruhusu kuwekwa hapo
ubavuni mwa Kanisa la Anglican Mkunazini ili yazidishe chuki juu ya Uislamu na Uarabu
kwani mwanamke huyu wa Kinordic alijua analolitaka na analolifanya. Ni msiba
mkubwa sana huu wa serikali yetu kutochukua tahadhari mapema juu ya mambo
yanaharibu ukweli wa historia ya nchi yetu. Ombi letu masanamu hayo yaondoshwe
haraka iwezekanavyo na uongo unaozuliwa kuhusu utumwa wa hapo Mkunazini
usimamishwe na uelezwe ukweli ya mahali hapo palivyokuwa Insha Allah Amin.
(Maelezo haya
yametolewa katika vitabu vya historia cha Prof. Roman Loirmier kiitwacho ‘’Between
Social Skilla and Marketable Skills The Politics of Islamic Education in 20th
Century Zanzibar).
No comments:
Post a Comment